Mtaalam
na Mkufunzi wa masuala ya Afya kutoka Makao Makuu ya Shirika la Afya
Duniani (WHO) Geneva,Switzarland Olau Poppe akitoa mafunzo kwa Timu ya
wataalam wa Afya kutoka nchi zipatazo 14 za Bara la Afrika kuhusu mfumo
wa taarifa unaotumika kutambua sababu za kifo cha mgonjwa kuwajengea
uwezo watalaam hao uelewa wa ujazaji wa taarifa sahihi juu ya sababu ya
kifo cha mgonjwa kwenye cheti cha kifo (Death Certificate) ili wakatoe
mafunzo kwa wataalam wengine kwenye nchi zao. Mafunzo hayo ya Siku mbili
yanafanyika jijini Dar es salaam.
Mtaalam
na Mkufunzi wa masuala ya Afya kutoka Makao Makuu ya Shirika la Afya
Duniani (WHO) Geneva, Olau Poppe akifuatilia majadiliano ya washiriki wa
mafunzo ya siku 2 ya wataalam wa Afya kutoka nchi zipatazo 14 za Bara
la Afrika kuhusu mfumo unaotumika kutambua sababu ya kifo cha mgonjwa
utakaowasaidia watalaam hao kujaza taarifa sahihi kwenye cheti cha kifo.
Mtakwimu
kutoka Makao Makuu ya Shirika la Afya Duniani (WHO) Geneva,Switzarland
Doris MA FAT (Kulia) akigawa machapisho yenye mwongozo kuhusu namna ya
kujaza taarifa mbalimbali zinazosababisha vifo wakati wa mafunzo ya siku
2 ya wataalam wa Afya kutoka nchi zipatazo 14 za Bara la Afrika leo
jijini Dar es salaam.
Baadhi
ya Washiriki wa mafunzo kwa Timu ya wataalam wa Afya kutoka Tanzania,
Zambia na Cameroon wakifuatilia miongozo mbalimbali iliyokuwa inatolewa
na watalaam kutoka Makao Makuu ya Shirika la Afya Duniani (WHO) wakati
wa Mafunzo kuhusu mfumo wa taarifa unaotumika kutambua sababu za kifo
cha mgonjwa kuwawezesha watalaam hao kujaza taarifa sahihi juu ya sababu
ya kifo cha mgonjwa leo jijini Dar es salaam.
PICHA/Aron Msigwa -MAELEZO
0 maoni:
Chapisha Maoni