Katibu
Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Bw. Uledi Mussa akiongea na wadau mbalimbali
wa uchumi nchini hawapo pichani wakati wa kufunga mkutano wa mwaka wa
mashauriano ya ushiriki wa watanzania Katika uwekezaji uliofayika jijini
Dar es salaam.
Katibu
Mtendaji wa Baraza la Taifa la uwezeshaji Wananchi Kiuchumi(NEEC) Bi.
Beng’i Issa akiongea na wadau mbalimbali wa uchumi nchini hawapo
pichani wakati wa kufunga mkutano wa mwaka wa mashauriano ya ushiriki wa
watanzania Katika uwekezaji uliofayika jijini Dar es salaam.
Mdau
wa Uchumi nchini na Mkurugenzi wa taasisi binafsi inayojihusisha na
biashara Namaingo Business Agency Bi. Biubwa Ibrahim akichangia hoja
wakati wa kufunga mkutano wa mwaka wa mashauriano ya ushiriki wa
watanzania Katika uwekezaji uliofayika jijini Dar es salaam.
Mdau
wa Uchumi nchini na Mkurugenzi wa Mfuko wa Bima (NIC) Bw. Sam Kamanga
akichangia hoja wakati wa kufunga mkutano wa mwaka wa mashauriano ya
ushiriki wa watanzania Katika uwekezaji uliofayika jijini Dar es salaam.
wadau
mbalimbali wa uchumi nchini wakifuatilia kwa makini majadiliano ya
wachngiaji mada wakati wa kufunga mkutano wa mwaka wa mashauriano ya
ushiriki wa watanzania Katika uwekezaji uliofayika jijini Dar es salaam.
……………………………………………………………………………
Na Ally Daud-Maelezo
Serikali
imesisitiza matumizi ya bidhaa za ndani ya nchi zinazotengenezwa na
watanzania ili kukuza uchumi wa nchi na kupanua ukubwa wa masoko ili
kuleta maendeleo.
Akizungumza
hayo wakati wa kufunga mkutano wa mwaka wa mashauriano ya ushiriki wa
watanzania Katika uwekezaji Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Bw. Uledi
Mussa amesema kuwa watanzania wajifunze kupenda na kutumia bidhaa za
ndani ili kuweza kuinua nchi kiuchumi kwa maendeleo ya Taifa letu.
“Ni
lazima watanzania tujifunze kubadilika kifikra na kimtazamo katika
kutumia bidhaa zilizopo nchini kuchangia Katika kukuza uchumi wa nchi
yetu ili kupiga hatua Katika maendeleo ya Tanzania”alisisitiza Bw.Uledi.
Aidha
Bw. Uledi amesema kuwa mwekezaji yeyote awe wa ndani au wa kigeni
anapaswa kutumia wafanyakazi wa nchini kama kama anataka kuwekeza Katika
Taifa letu ili kutoa fursa kwa watanzania kushiriki Katika kuinua
uchumi.
“Mwekezaji
wa kigeni au wa ndani inampasa atumie wataalamu na wafanyakazi wa
Tanzania kama anataka kuwekeza nchini mwetu ili vijana wetu wa
kitanzania wapate fursa ya kuchangia Katika kuinua uchumi wa
nchi”.aliongza Bw. Uledi.
Mbali
na hayo Bw. Uledi Mussa amesema kuwa kiwanda chochote kinachowekeza
nchini wanapaswa kutumia malighafi kutoka Tanzania ili kuweza kupiga
hatua kimaendeleo Katika Taifa letu kwa ujumla.
Naye
Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la uwezeshaji Wananchi
Kiuchumi(NEEC) Bi. Beng’i Issa amesema kuwa Katika mkutano huo wenye
kauli mbiu ya “Ongeza Ushiriki Inua Uchumi” umetoka na mkakati wa
kuhakikisha makampuni yote ya uwekezaji kutoka nje yajiandikishe Katika
soko la Hisa (DSE) ili kuongeza ushirikina umiliki wa watanzania Katika
makampuni husika.
Aidha
bi. Issa ameongeza kuwa mkutano huo umelenga kuwa wakandarasi wote
ambao wa ndani wanapewa malipo yao kwa wakati kama walivyokubaliana ili
kumsaidia mtanzania kushiriki Katika kukuza uchumi wa nchi.
0 maoni:
Chapisha Maoni