………………………………………………………………………………………..
Na Ally Daud-Maelezo
Chuo Kikuu Ardhi kimetakiwa
kubuni majengo ya shule kwa kiwango kikubwa na teknolojia ya sasa ili
kuweza kupata majengo imara na usanifu mkubwa nchini kwa ajili ya
maendeleo ya elimu kwa wasomi wa ndani.
Akizungumza hayo Waziri wa Elimu ,
Sayansi , teknolojia na mafunzo ya Ufundi Prof. Joyce Ndalichako
wakati wa ufunguzi wa maonesho ya 11 ya elimu ya juu , sayansi na
teknolojia na kutembelea banda la chuo hiko amesema kuwa wana uwezo wa
kubuni majengo hivyo wajitahidi na kuwakilisha kwake.
“Kwa kuwa mmeweza kunionyesha
baadhi ya ubunifu wa majengo katika banda lenu basi nawaomba muendelee
na kubuni majengo ya shule kwa usanifu mkubwa ili yatusaidie kukuza
elimu nchini” aliongeza Prof. Ndalichako.
Katika maonyesho hayo yalioanza
leo na kufikia tamati Julai 22 mwaka huu banda la Chuo kikuu Ardhi kina
baadhi ya michoro ya majengo yaliyobuniwa na wanafunzi wa chuo hiko na
ramani mbalimbali za majengo.
0 maoni:
Chapisha Maoni