Mkuu
wa mkoa wa Mbeya Amos Makalla ametembelea eneo la Pandahill kata ya
Songwe mahali ambapo patachimbwa madini adimu aina ya Niobium ambayo
hutumika kutengeneza Ndege na computer.
Mpaka
sasa madini hayo huchimbwa bara la Amerika tu na kugundulika kwa madini
hayo Tanzania utakuwa mgodi wa nne duniani na wa kwanza Afrika
Mkurugenzi
wa kampuni ya Pandahil limited ndg Derick amesema imewachukua zaidi ya
miaka 5 kufanya utafiti na kugundua uwepo wa madini hayo, taratibu zote
za kisheria zimekamilika na kampuni hiyo itawekeza zaidi ya shilingi
bilioni 500 katika mradi huo na mradi utatengeneza ajira watu 500 na
mradi huo utaanza uzalishaji mapema mwaka 2018.
Mkuu
wa mkoa ameipongeza kampuni hiyo kwa ugunduzi na uwekezaji huo mkubwa
sanjali na kuwataka na kutoa ushirikiano na ushirikishwaji wa kwa
viongozi na wananchi kwa kila hatua ili kuweka wazi mradi huo kwa
wananchi.
Aidha
amewataka wananchi na viongozi kutoa ushirikiano kwa kampuni hiyo ili
wananchi wanaozunguka eneo hilo uzalishaji utakapoanza wafaidike na
ajira, huduma za jamii na kodi mbalimbali kwa hslmashauri na serikali
kuu
Pia amewashukuru kwa mchango wa madawati 400 ambayo yatasambazwa kwa shule 7 zilizokuwa na upungufu wa madawati
Hata
hivyo Gereza la Songwe mkoani Mbeya linatalaji kuvunjwa na kuhamishiwa
sehemu nyingine kupisha uchimbaji wa madini hayo adhimu ya duniani ya
niobium baada ya madini hayo kugundulika kuwepo karibu na maeneo ya
gereza hilo la songwe.
Kwa
mujibu wa taarifa za wataalam zinadai kuwa madini ya mgodi huo
huchanganywa na metali zingine na vyuma vyake hutumika kwenye ujenzi
bomba la kupitishia mafuta sanjali na metali zake kutumika katika injini
za ndege ili kuzuia mitambo yake kutopata joto kali.
| Ramani ya mradi. |
| Eneo ambalo litahusika kwa ajili ya uchimbaji wa madini ya adimu aina ya Niobium ambayo hutumika kutengeneza Ndege na computer katika eneo la Songwe Gerezani Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya. |






0 maoni:
Chapisha Maoni