Mahakama
nchini Afrika Kusini imemhukumu mwanariadha wa nchi hiyo, Oscar
Pistorius kifungo cha miaka sita kwa kosa la kumuua kwa kudhamiria
aliyekuwa mpenzi wake, Reeva Steenkamp mwaka 2013.
Hatia
ya Pistorius kukutwa na kosa hilo ilitolewa mwaka jana mwezi Disemba
baada ya majaji kukutana na kujadili kifo cha Reeva kilivyotokea na
kutoa uamuzi wa kuwa kifo hicho nicha kudhamiria na hivyo kesi yake
kubadilishwa kutoka kosa la kuua bila kudhamiria hadi kuua kwa
kudhamiria na hivyo kesi kutakiwa kutolewa hukumu upya.
Baada
ya huku kutolewa Pistorius amepelekwa moja kwa moja gerezani na upande
wa mshitaki na utetezi wanaruhusiwa kukata rufaa ya kesi hiyo lakini
mawakili wa Pistorius wamesema kuwa wao hawataka rufaaa hivyo ni wazi
mteja wao atakwenda kutumikia kifungo cha miaka sita gerezani labda tu
kama atatumia mawakili wengine.
Ikumbukwe Pistorius alimpiga risasi nne aliyekuwa mpenzi wake, Reeva Steenkamp, Februari 2013 kwa madai kuwa akijua ni muharifu






0 maoni:
Chapisha Maoni