Zikiwa
zimesalia siku kadhaa kabla ya kusherekea sikukuu ya Eid El Fitri,
Kampuni ya Multichoice Tanzania ambao ndiyo wasambazaji wa ving’amuzi
vya DSTV nchini imetoa msaada wa vitu mbalimbali kwa watoto yatima ambao
wanaishi katika kituo cha Al-Madina kilichopo Tandale kwa Tumbo,
misaada ambayo kwa namna moja au nyingine inaweza kusaidia kubadilisha
maisha ya watoto hao.
Misaada
ambayo imetolewa kwa watoto hao ni Cherehani 4, kapeti 12, vikombe 60,
sahani 40, magodoro 11, shuka 40, tenga za nguo 3, jagi 6, beseni kubwa
3, sufuria 9, chupa za chai 4 na mikeka 6.
Akizungumzia
misaada hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa Multichoice Tanzania, Maharage
Chande alisema msaada huo ni mwendelezo wa misaada ambayo Multichoice
imekuwa ikitoa kwa kituo hicho kwa lengo la kuwasaidia kuishi maisha
bora lakini pia kuwapatia msaada ambao unaweza kuwasaidia kuwa na uwezo
wa kuingiza kipato.
Mkurugenzi Mtendaji wa Multichoice Tanzania, Maharage Chande akizungumza kuhusu msaada ambao wameutoa kwa kituo cha Al–Madina.
“Multichoice
tumekuwa tukitoa misaada yetu kwa kituo hiki tangu 2009 na leo
tumewaletea mwingine ikiwa ni kila mwaka tunafanya hivyi lakini kwa
mwaka huu tumeleta pia Cherehani ambazo zitawasaidia kupata kipato,
“Pamoja
na hayo pia tumewafungia king’amuzi ambacho watoto watakuwa wakiangalia
vipindi balimbali baada ya kurejea nyumbani na tuna chaneli mbalimbali
za vipindi vya watoto na burudani kwahiyo tunaamini kuwa watoto
watafurahi,” alisema Chande.
Nae
mlezi wa kituo hicho, Bi. Kuruthum Yusuf aliwataja Multichoice kama
kampuni ambayo imekuwa mstari wa mbele kuwapatia misaada na kuyaomba
makampuni mengine kuwa na utaratibu kama wa Multichoice wa kuwasaidia
misaada kutokana na kuwa na idadi kubwa ya watoto ambao wanahitaji
misaada ili kuboresha maisha yao.
Mlezi
wa kituo cha watoto yatima cha Al-Madina akizungumza kuhusu msaada
ambao wamepokea na jinsi ambavyo Multichoice Tanzania imekuwa ikiwapatia
misaada. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Multichoice Tanzania,
Mharage Chande.
“Tangu
walipotufahamu wamekuwa wakitupatia misaada kila mwaka, niwashukuru
sana kwa moyo wao na kutoa sio utajiri ila tu wana moyo wa kutoa na hata
wenngine wanatakiwa kuwa na moyo kama wao (Multichoice) wa kusaidia,”
alisema Bi. Kuruthum.
Pamoja
na hayo pia, Bi. Kuruthum alieleza kuwa kwa sasa bado wanakabiliwa na
changamoto ya vifaa vya shuleni kwa watoto ambao wanasoma.
Kutokana
na msaada ambao umetolewa na Multichoice kwa watoto wa kituo cha
Al-Madina ambacho kina watoto 57, wasichana wakiwa ni 23 na wavulana ni
34 basi ni wazi kuwa kama wakitumia msaada huo vyema basi kwa namna moja
au nyingine wanaweza kubadilisha maisha yao kwa hatua fulani ambayo
awali hawakuwa nayo kama vile kutumia cherehani kwa kushona nguo na
kujiongezea kipato.
Meneja
Uhusiano na Masoko wa Multichoice Tanzania, Furaha Sumalu akitoa neno
la ufunguzi kuhusu misaada ambayo imekuwa ikitolewa na Multichoice
Tanzania pamoja na historia fupi ya kituo hicho.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Multichoice Tanzania, Mharage Chande akimkabidhi Cherehani,
mlezi wa kituo cha Al-Madina, Kuruthum Yusuf. Wa tatu kushoto ni Meneja
Uhusiano na Masoko wa Multichoice Tanzania, Furaha Samalu wakiwa na
wafanyakazi wengine wa Multichoice Tanzania.
Meneja
Uhusiano na Masoko wa Multichoice Tanzania, Furaha Samalu
akimpongeza mlezi wa kituo cha Al-Madina, Kuruthum Yusuf baada ya
kukabidhiwa misaada na Multichoice Tanzania.
Wafanyakazi wa Multichoice Tanzania wakiwa katika picha ya pamoja na watoto yatima wanaoishi katika kituo cha Al-Madina.
Meneja Uhusiano na Masoko wa Multichoice Tanzania, Furaha Samalu akiwaelekeza jambo watoto wanaoishi katika kituo cha Al-Madina.
Watoto yatima wanaoishi katika kituo cha Al-Madina wakiwa katika picha ya pamoja.
Mwonekano wa vitu vilivyotolewa na Multichoice Tanzania kwa kituo cha kulelea watoto yatima cha Al-Madina.
0 maoni:
Chapisha Maoni