Watu
mbalimbali ambao wamejitolea katika taasisi ya Gulf for Good wakiwa
pamoja na watoto ambao watanufaika na mpango wa Larchfield. Gulf for
Good ni taasisi ambayo inahusisha watu mbalimbali ambayo imekuwa
ikifanya kazi ya kusaidia kutatua baadhi ya changamoto zinazozikabili
jamii katika maeneo mbalimbali duniani.
Watu
mbalimbali ambao wamejitolea katika taasisi ya Gulf for Good wakiwa
pamoja na watoto ambao watanufaika na mpango wa Larchfield ambao
unalengo la kuwasaidia watoto yatima na wanaotoka katika mazingira
magumu wakiwa wamevalia sare ambazo wamepewa na Taasisi ya Misaada ya
Larchfield.
Watu
mbalimbali ambao wamejitolea katika taasisi ya Gulf for Good
wakiwagawia vifaa vya shule watoto ambao watafaidika na mpango wa
Larchfield.
Kwa
kutambua umuhimu wa elimu, Taasisi ya Misaada ya Larchfield imeanzisha
mpango unaofahamika kwa jina la Larchfield ambao utawezesha watoto 300
kupataelimu bure kutoka wilaya ya Mkuranga, Pwani.
Mpango
huo umeanzishwa ukiwa na malengo ya kuwasaidia watoto ambao ni yatima
na ambao wametengwa na ndugu ambao wazazi wao wameshafariki au
wasiojiweza kiuchumi ili kuwasomesha watoto wao na mpango huo utahusika
na watoto walio na umri kati ya miaka 3-16.
Katika
taarifa ambayo imetolewa na taasisi ya Larchfield ilieleza kuwa kwa
takwimu zilizopo nchini zinaonyesha kuwa Tanzania ina wananchi milioni
1.5 ambao wanaishi na UKIMWI na watoto yatima wanakadiliwa kufikia
milioni 1.3 hivyo ujio wa mpango huo utawasaidia karibu watoto yatima
2,000 ambao wanapatikana wilayani Mkuranga.
Katika
kuwasaidia watoto hao, taasisi ya Larchfield imejipanga kuhakikisha
inarudisha furaha iliyopotea kwa watoto, kuwaboreshea usalama na ulinzi
wa mazingira ambayo yanawazunguka na katika utekelezaji wa azma hiyo
hawatafanya ubaguzi wa rangi au kijinsia au dini.
Aidha
katika kuzindua mpango huo, walipata ugeni wa watu ambao wanajitolea
kufanya kazi na Taasisi ya Gulf For Good ambalo walijumuika nao Mkuranga
katika uzinduzi na kupata nafasi ya kuzungumza na wafaidika wa mpango
huo.
Kwa
kuanza utekelezaji wa mpango huo ulio na malengo ya kuwasomesha watoto
300, kutakuwa na awamu na kwa awamu ya kwanza watasomeshwa watoto 50 na
kiasi cha fedha cha Dolla ya Kimarekani 275,000 kinataraji kutumika.
0 maoni:
Chapisha Maoni