Waziri
wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu)
Mhe. Jenista Mhagama ameizindua rasmi Bodi ya Wadhamini wa Hifadhi ya
Jamii wa NSSF Julai 5, 2016 Dar es Salaam.
Bodi
hiyo imezinduliwa rasmi na kujadili mambo muhimu ikiwa ni kufikia
malengo ya mfuko huo kwa kuzingatia masuala ya Utawala bora na
ushirikiano ili kuchangia kukua kwa uchumi wa wananchi na kusaidia
mahitaji ya wanachama wa mfuko huo.
Mhe.Mhagama
aliahidi kutoa ushirikiano wake kwa Bodi hii mpya ili kusaidia majukumu
yote na kuhakikisha mafanikio yaliyopo yanakuwa ni chachu ya kuongeza
kasi ya kufanya vizuri zaidi ili kuifikisha mahali pazuri zaidi.
“Ninawaahidi
kuwapa ushirikiano wa hali na mali na kuamini kuwa Prof.Wangwe
ameaminiwa na kupewa dhamana ya kutufikisha mahali fulani kwa kuisaidia
bodi hii iliyozinduliwa rasmi leo.”Alisisitiza Mhe.Mhagama.
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu)
Mhe. Jenista Mhagama (mb) akisisitiza jambo wakati wa mkutano wa
uzinduzi wa Bodi ya Wadhamini ya Mfuko wa Hifadhi ya Jamii NSSF
uliofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Ofisi ya Waziri Mkuu Julai, 05,
2016.
Kwa
upande wake Mwenyekiti wa Bodi hiyo Prof.Samwel Chacha Wangwe alieleza
kuwa, watajikita kwa kusaidia maeneo muhimu yenye changamoto kwa
kuhakikisha wanaboresha na kuongeza wanachama wa Mfuko huo.
“eneo
la Utawala bora utakuwa msingi wa kusaidia mfuko uwe imara kwa
kuzingatia kuwapa kipaumbele wanachama ili kuendana na kasi ya kukuza
uchumi kwa kuzingatia kaulimbiu ya hapa kazi tu” Alisema Prof.Wangwe.
Mhe.Mhagama
alimalizia kwa kuwashukuru wajumbe wote kwa kufika na kushiriki katika
uzinduzi huo, “nitoe shukrani zangu za dhati kwa wajumbe wote na
kuwaomba tuwe kitu kimoja ili kuhakikisha shirika linatumia rasilimali
zake ipasavyo ili kuwa na mapato ya kutosha.” Alisisitiza Mhe. Mhagama.
Baadhi
ya wajumbe wa Bodi ya Wadhamini ya Mfuko wa Hifadhi ya Jamii NSSF
wakimsikiliza Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na
Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama (hayupo pichani) wakati wa
uzinduzi wa bodi hiyo katika Ukumbi wa Mikutano wa Ofisi hiyo Julai 5,
16 Dar es Salaam.
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu)
Mhe. Jenista Mhagama akimkabidhi vitendea kazi Mwenyekiti wa Bodi ya
Wadhamini ya Mfuko wa Hifadhi ya Jamii NSSF Prof. Samwel Chacha Wangwe
mara baada ya uzinduzi wa bodi hiyo Julai 5, 2016.
Mwenyekiti
wa Bodi ya Wadhamini ya Mfuko wa Hifadhi ya Jamii NSSF Prof. Samwel
Chacha Wangwe akitoa neno la shukrani kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri
Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama
(hayupo pichani) mara baada ya uzinduzi wa Bodi hiyo Julai 05, 2016
katika Ukumbi wa Ofisi ya Waziri Mkuu.
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu)
Mhe. Jenista Mhagama (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe
wa Bodi ya Wadhamini wa Mfuko wa Hifadhi wa Jamii (NSSF) mara baada ya
kuuzindua rasmi katika Ofisi yake Jijini Dar es Salaam.(PICHA ZOTE NA
OFISI YA WAZIRI MKUU).






0 maoni:
Chapisha Maoni