Naibu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Watoto na Wazee, Dkt. Hamisi
Kigwangalla akitoa maelezo namna ya miundo ya Hospitali na viwango
vyake..
Picha ya jengo hilo la Hospitali pindi litakapokamilika
Muonekano wa mbali katika jengo hilo la kanisa
Heshima zikitolewa kwa mgeni rasmi
Matembezi ya sherehe hiyo yakiendelea
Sehemu ya umati wa watu katika tukio hilo la Jubilee ya Miaka 50
Vikundi vya matembezi yakiendelea
Jukwaa kuu wakishuhudia matembezi hayo
Naibu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Watoto na Wazee, Dkt. Hamisi
Kigwangalla akielekea kukagua gwaride la vijana hao
Vijana PF wakipita kwa mwendo wa haraka mbele ya mgeni rasmi (Hayupo pichani)
| Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Watoto na Wazee, Dkt. Hamisi Kigwangalla akihutubia katika tukio hilo |
| Add caption |
Vijana wakiwa katika hali ya ukakamavu katika tukio hilo Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Watoto na Wazee, Dkt. Hamisi Kigwangalla akihutubia katika tukio hilo
Naibu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Watoto na Wazee, Dkt.
Hamisi Kigwangalla amesema Serikali itaendelea kushirikiana na taasisi
mbalimbali za watu binafsi zikiwemo zile za kidini na kijamii katika
kufanikisha maendeleo ambapo amelipongeza Kanisa la Waadventista wa
Sabato la Ilemela Jijini Mwanza kwa hatua yake kujenga Hospitali ya
Kisasa ambayo itakuwa msaada katika Wilaya hiyo.
Dk.
Kigwangalla ambaye alikuwa mgeni rasmi katika tukio hilo la ufungaji wa
sherehe za miaka 50 ya Jubilee ya kuanzishwa Utume wa Kanisa la
Waadventista wa Sabato katika jiji la Mwanza tukio lililofanyika siku ya
Julai 3.2016 kwenye uwanja wa CCM Kirumba.
Akitoa
hotuba za kufunga sherehe hizo, Dk. Kigwangalla amelipongeza kanisa la
Kirumba kuwa na jubilee ya miaka 50 Lakini pia amelipongeza kwa huduma
ya malezi ya vijana wa kanisa hilo wakingali wadogo na kwamba kwa
kufanya hivo ni kuliandaa kanisa na Taifa kwa ujumla kuwa na viongozi
waadilifu.
Dk. Kigwangalla ameyataka madhehebu ya dini yawe mstari wa mbele katika kukemea maovu ili Taifa lidumu kuwa na Amani.
“Uwepo
wenu tunaupongeza kwani naamini mumekuwa mstari wa mbele katika
kuliombea Amani Taifa hili na pia kuwaombea ulinzi watu mbalimbali
pamoja na kutoa misaada, huduma za Afya na mambo mengine mbalimbali. Hii
ni faraja sana na Serikali tutaendelea kuwaunga mkono.
Aidha,
katika hutuba hiyo, Dk. Kigwangalla aliwahakikishia uongozi wa kanisa
hilo kuwa Hospitali yao mpya inayojengwa Serikali itakuwa nao bega kwa
bega na kuaahidi kutoa ushirikiano katika suala hilo la ujenzi pamoja
na uendeshaji wa Hospitali hiyo kwa lengo la kuboresha afya za Wananchi
wote.
Katika
hatua nyingine, Dk. Kigwangalla alikemea vitendo vilivyoanza kushamili
ikiwemo baadhi ya watu kushabikia masuala ya mapenzi ya jinsia moja
ambapo ikiwemo suala la ushoga.
“Serikali
haipo tayari kuona vitendo vya ushoga vinafanyika kwa wananchi wake
lakini pia kuzitangaza kwa jamii. Wizara yangu itakutana na NGOs, zote
za Kijamii na taasisi zilizosajiliwa ambazo pia zingine zipo chini ya
Wizara yetu kukaa nazo na kujua ni zipi zinajihusisha na masuala haya
iwe kwa kutetea ushoga ama kubariki vitendo hivi, tutawachukulia hatua
kali za kisheria na hata kuzifuta kabisa” alimalizia Dk. Kigwangalla.
Aidha,
katika tukio hilo, Dk. Kigwangalla alipata kutembelea ujenzi wa
Hospitali hiyo mpya na ya kisasa inayotarajiwa kukamilika kwake hapo
baadae na kisha kuwasili kwenye viwanja vya CCM Kirumba ambapo pia
alipata kukagua gwaride la vijana wadogo, wa kati na wa kanisa hilo
ambao ni pamoja na vijana waliopatiwa mafunzo ya
Kiroho, Kimwili na Kikakamavu wakiwemo Wavumbuzi (adventure) Watafuta
njia (path finder-Pf), Mabalozi na Kiongozi Mkuu (Master Guide)






0 maoni:
Chapisha Maoni