Kocha
Mkuu wa timu ya Taifa ya Vijana wenye umri wa chini ya miaka 17
‘Serengeti Boys’, Bakari Nyundo Shime, amesema hatarajii kuwa na
mabadiliko makubwa ya kikosi katika mchezo dhidi ya vijana Shelisheli
utakaopigwa kesho Jumamosi Julai 2, 2016 kwenye Uwanja wa Stade Linite
mjini Victoria.
“Timu
haitakuwa na mabadiliko makubwa. Almost kikosi kitakuwa ni kilekile cha
Dar es Salaam kwa sababu nitampumzisha Job (Dickson Nickson) tu katika
mchezo wa kesho, na nafasi yake atacheza Enrick (Vitalis Nkosi),”
amesema Shime leo Julai 1, 2016 kabla ya kwenda kwenye mazoezi ya mwisho
yatakayofanyika Uwanja wa Linite.
Shime
maarufu kwa jina la Mchawi Mweusi, amesema anauchukulia mchezo huo kwa
uzito uleule na kuongeza ana sababu za kiufundi na kimbinu kumpumzisha
Job katika mchezo wa marudiano kuwania nafasi ya kufuzu fainali za Kombe
la Mataifa ya Afrika kwa vijana, zitakazofanyika mwakani huko
Madagascar.
Kwa
hali halisi ilivyo timu iko vema na ikathibitishwa na Shime mwenyewe
akisema: “Kikosi kiko vema kwa maana ya wachezaji wako vizuri na kambi
iko vizuri kwa sababu hakuna majeruhi.” Pia Daktari wa timu hiyo, Shecky
Francis Mngazija alithibitisha.
“Sioni
kama kuna dalili zozote za hujuma na kimbinu tumejipanga vema. Tumefuta
matokeo ya Dar na tuko huku tunataka matokeo mapya. Mbinu zangu siku
zote ni ushindi wa nyumbani na ugenini,” amesisitiza.
Serengeti
Boys ilitua kwenye Kisiwa cha Mahe uliko Uwanja wa Ndege wa Kimataifa
wa Visiwa vya Shelisheli jana Juni 30, 2016 majira ya saa 11 jioni.
Timu
hiyo iliyosafiri kwa ndege ya Shirika la Ndege la Ethiopia ilisafiri
salama na wachezaji wote 20 wakiwa na viongozi wanane, walikuwa kwenye
hali nzuri na kupokewa vema na wenyeji waliowaandalia usafiri kutoka
uwanjani hapo hadi Victoria- Mji Mkuu wa nchi hii na kufikia Hoteli ya
Berjaya Beau Vallon Resort iliko Kilometa 25 kutoka uwanja wa ndege.
Leo
Julai mosi, itakuwa na mazoezi ya kipindi kimoja tu kwenye uwanja huo
kuanzia saa 10.30 jioni (saa 9.30 kwa saa za Tanzania au Afrika
Mashariki). Uwanja wa Stad Linite upo kilometa 10 kutoka hotelini.
Shime
ana matumaini makubwa kuiondoa Shelisheli katika mbio hizo baada ya
kuvuna ushindi mnono wa mabao 3-0 katika mchezo wa kwanza uliofanyika
Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, Jumapili ya Juni 26, 2016.
Na
ili iweze kufuzu, Serengeti Boys inahitaji kusimama imara katika
matokeo hayo ama kwa kupata sare ya aina yoyote, kushinda au ikitokea
kupoteza, basi isifungwe zaidi ya mabao 2-0.
Katika
mchezo wa Dar es Salaam waliozifumania nyavu walikuwa Nickson Kibabage,
Ibrahim Abdallah na Ally Hussein ambaye alifunga kwa penalti na kila
mmoja amepania kufunga kama kocha akiwapa nafasi ya kuanza katika kikosi
cha kwanza.
Nyota
waliosafiri ni pamoja na makipa, Ramadhani Awm Kabwili na Samwel Edward
Brazio wakati mabeki wako Kibwana Ally Shomari, Nickson Clement
Kibabage, Israel Patrick Mwenda, Dickson Nickson Job, Ally Hussein
Msengi, Issa Abdi Makamba.
Viungo
ni Kelvin Nashon Naftal, Ally Hamisi Ng’anzi, Asadi Ali Juma Ali,
Syprian Benedictor Mtesigwa, Ibrahim Abdallah Ali, Yassin Muhidini
Mohamed, Shaban Zuberi Ada huku washambuliaji wakiwa ni Rashid Mohammed
Chambo, Mohammed Abdallah Rashid, Yohana Oscar Mkomola, Muhsin Malima
Makame Vitalis.
Serengeti
Boys ambayo inahudumiwa na TFF kwa asilimia 100 ilikuwa kambini tangu
Juni 14, 2016 kujiandaa na mechi hizo za kufuzu fainali za Kombe la
Mataifa ya Afrika dhidi ya Shelisheli na Afrika Kusini ambayo itapambana
nayo baadaye mwezi ujao.
Katika
kuajindaa na mchezo huo, Serengeti Boys ilifanya ziara India ambako
walishiriki mashindano ya vijana ya Kimataifa yanayotambuliwa na FIFA
(AIFF International Youth Tournament 2016) kabla ya kurudi na rekodi ya
kupigiwa mfano si tu katika Tanzania na kwa nchi za Afrika Mashariki.
Ilishika nafasi ya tutu nyuma ya Korea Kusini na Marekani.
0 maoni:
Chapisha Maoni