Mtangazaji wa
Choice Fm cha Dar es Salaam, Jimmy Kabwe (katikati), akizungumza na
waandishi wa habari jijini Dar es Salaam wakati wa hafla yakuingia
makubaliano kati ya Timu ya mpira wa miguu ya African Lyon inayoshiriki
ligi kuu Tanzania Bara (Vodacom Premier League) na kituo cha radio cha
Choice FM 102.5, juu ya ushirikiano katika kukuza vipaji na kuboresha
misingi ya uendeshaji wa timu, wengine kushoto kwake alievaa kanzu ni Mmiliki wa klabu ya African Lyon, Rahim Kangezi, na Mkuu wa Vipindi Choice FM, Antonio Nugaz, Mkuu wa Masoko na Mauzo wa Choice FM .Mkuu wa Vipindi Choice FM, Antonio Nugaz (kulia) akitolea ufafanuzi makubaliano hayo ambapo amesema yanalenga kujenga mazingira ya kuweza kutambua na kuvikuza vipaji vya wanamichezo hasa wale wa mpira wa miguu (kushoto), Mmiliki wa klabu ya African Lyon, Rahim Kangezi
Amesema makubaliano hayo yataiwezesha Africani Lyon yenye masikani yake Mbagala kushirikiana na Choice FM katika kuandaa mashindano na programm zinginezo ambazo zitaleta mvuto kwa vipaji vya wanamichezo wa Kike na Kiume.
Mmiliki wa klabu ya African Lyon, Rahim Kangezi (katikati), akitoa neno la shukrani kwa kituo cha radio cha Choice FM 102.5 mara baada ya kuingia makubaliano .
Mmiliki wa klabu ya African Lyon, Rahim Kangezi, na Captain African
Lyon, Baraka Jafari (Nyaka) wakikabidhiwa jezi wakati wa hafla
yakuingia makubaliano kati ya Timu ya mpira wa miguu ya African Lyon
inayoshiriki ligi kuu Tanzania Bara (Vodacom Premier League) na kituo
cha radio cha Choice FM 102.5, juu ya ushirikiano katika kukuza vipaji
na kuboresha misingi ya uendeshaji wa timu.
PICHA ZOTE NA PHILEMON SOLOMON-FULLSHANGWEBLOG
0 maoni:
Chapisha Maoni