Jumanne, 5 Julai 2016

AJALI YA MOTO YATEKETEZA MABWENI MATATU KITUO CHA KULEA WATOTO YATIMA FARAJA MGONGO IRINGA


 
Dc kasesela akishirina na jeshi la zima moto na wananchi katika jitihada za kuuzima moto 
Dc akuzungumza na watoto walioathirika na ajali hiyo,baada ya vifaa vyao kuungua na moto
Dc kasesela akizungumza na wananchi waliojitokeza kuzima moto
Moto wateketeza mabweni matatu katika kituo cha kulea watoto yatima kilichopo eneo la Mgongo Nduli Manispaa ya Iringa, usiku wa kuamkia leo. 
Mkuu wa wilaya ya Iringa Mh Richard Kasesela akizungumza na wananchi baada ya tukio la kuzima moto kumalizika alisema Moto huo ulisababishwa na hitilafu ya umeme na kuteketeza mabweni 3, pamoja na mali za watoto hao zikiwemo nguo, madaftari na magodoro.
   ''''''Nilipata taarifa nikiwa kwenye hafla ya futari iliyo andaliwa na Benki ya CRDB ikabidi niache nije mara moja nafurahi kuona tumefanikiwa kuzima moto ingawa umeleta madhara makubwa kwa wanafunzi wanaolelewa katika nkituo hicho.'''''alisema Kasesela
 '''''Tunakishukuru Kikosi cha zimamoto chini ya Mrakibu Komba,baada ya kupata taarifa tu walifika eneo la tukio na kufanya kazi ya ziada kuzuia moto kwa kushirikiana na wananchi wa eneo hili nahatimae tukaokoa baadhi ya mabweni ambayo yalikuwa bado hayajaathirika na moto huo''''alisema.
 Kasesela alisema inakadiriwa watoto zaidi ya 45 wameathirika na moto huo, na hakuna majeruhi hata mmoja.Amewaomba wadau wajitokeze kusaidia vifaa mbalimbali kwa ajili ya watoto waliopatwa na maafa hayo ikiwemo magodoro,Daftari, blanketi na nguo hasa ukizingatia kipindi hiki ni cha baridi.

0 maoni:

Chapisha Maoni