Mbunge
wa Nzega Vijijini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya
Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dk. Hamisi Kigwangalla amewaomba
wananchi wa Kijiji cha Ipala ambao wamekuwa na mgogoro wa muda mrefu na
watu hifadhi ya Msitu wa Ipala kuwa na subira kwa kipindi hiki kwani
tatizo lao linashughulikiwa ambapo Waziri mwenye dhamana anatarajiwa
kufika kwenye kijiji hicho kwa ajili ya hatua Zaidi za kitatuzi.
Kijiji
hicho cha Ipala chenye Zaidi ya Kaya 700, Wanakijiji wake wamekuwa
wakiishi huko kuanzia mwaka 1952 ambapo wameendelea kuishi humo na
familia na kufanya shughuli zao za kijamii za kila siku Dk. Kigwangalla
amesema kuwa, tayari Serikali suala hilo wanalitambua hivyo wanatumia
njia za mazungumzo katika kutatua mgogoro huo kwa sasa wanatarajia ujio
wa Waziri Mwenye dhamana kutembelea eneo hilo.
“Matatizo
yenu nayajua na Serikali pia inalifahamu suala hili muda mrefu hivyo
nawaomba wananchi muwe na subira kwa kipindi hiki na mimi Mbunge wenu
natarajia kurudi hapa na Mh. Waziri wa Maliasili na Utalii na atafika
huku kuja kushuhudia mgogoro huu.” Alieleza Dk. Kigwangalla kwa wananchi
hao huku akishangiliwa na wanakijiji hao waliofurika kwa wingi katika
eneo la uwanja wa kituo cha Ipala.
Mbunge
wa Nzega Vijijini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya
Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dk. Hamisi Kigwangalla akiwasili
kwenye kijiji cha Ipala huku akipokelewa na baadhi ya wananchi wa vijiji
hivyo
Msululu wa wananchi wakiwa wamempokea Dk. Kigwangalla wakati akiwasili kwenye kijiji cha Ipala.
Mbunge
wa Nzega Vijijini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya
Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dk. Hamisi Kigwangalla akizungumza
na badhi ya wananchi wa Kijiji cha Ipala. Dk. Kigwangalla amewataka
wananchi hao kuendelea kusubiria kwani tatizo hilo analitatua kwa njia
ya mazungumzo na tayari Waziri mwenye dhamana amekubali kufika eneo hilo
kwa ajili ya kujionea. (Picha zote na Andrew Chale,Nzega-Tabora).
0 maoni:
Chapisha Maoni