Kwa
muda mrefu Tanzania imekuwa na urafiki na Korea na katika kulidumisha
hilo, Balozi wa Korea nchini, Song Geum-young amemtembelea Naibu Waziri
wa Afya, Ustawi wa Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Hamisi
Kigwangalla na kuzungumza mambo mbalimbali kuhusu ushirikiano wa Korea
na Tanzania zaidi katika sekta ya afya na jinsi Korea ambavyo imekuwa
ikisaidia uboreshwaji wa huduma za kiafya nchini.
Akizungumza
na Mo Blog kuhusu ugeni huo, Dk. Kigwangalla alisema kuwa balozi
Geum-young alitaka kujua kama naibu waziri anafahamu kuhusu ujenzi wa
chuo na hospitali ya Mlonganzira ambapo alitaka kufahamu kama serikali
itakuwa tayari kutoa watumishi wa afya 900 ambao watahudumia hospitali
hiyo.
Naibu
Waziri wa Afya, Ustawi wa Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Hamisi
Kigwangalla akizungumza na balozi wa Korea nchini, Song Geum-young
kuhusu uhusiano wa Tanzania na Korea na jinsi ambavyo nchi hiyo imepanga
kuendelea kuisaida Tanzania katika kuboresha huduma za kiafya nchini.
(Picha zote na Rabi Hume, MO Blog)
Katika
hilo Dk. Kigwangalla alimuhakikishia balozi kuwa serikali ipo tayari
kutoa wataalam wa afya ambao watakuwa wakitoa huduma katika hospitali ya
Mlonganzira ambayo itakuwa na vifaa vya kisasa kutoka Korea na itakuwa
na vitanda 600 ambavyo vitakuwa vinatumiwa na wagonjwa wanaofika kupata
huduma.
Naibu
Waziri wa Afya, Ustawi wa Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Hamisi
Kigwangalla akifanya mazungumzo na balozi wa Korea nchini, Song
Geum-young, alipofika ofisini kwake kwa ajili ya kuzungumza mambo
yanayohusu mahusiano ya Tanzania na Korea.
Jambo
lingine ambalo walizungumza ni kuhusu msaada wa magari ya kutolea
huduma za kiafya ambayo yanatembea ‘mobile clinic’ ambayo yatatolewa kwa
kanda zote nchini na zaidi katika maeneo ambayo yanaonekana kuwa na
ugumu kufikika na kuwa na vituo vya afya vichache.
Naibu
Waziri wa Afya, Ustawi wa Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Hamisi
Kigwangalla akizungumza na balozi wa Korea nchini, Song Geum-young, wa
kwanza kushoto ni Katibu wa Balozi wa Korea, Songwon Shin na wapili
kulia ni Katibu wa Naibu Waziri wa Afya, Ustawi wa Jamii, Jinsia, Wazee
na Watoto, Kulwa.
“Amesema
watatuletea convoy zaidi ya sita (kila moja ina magari 10) ambayo
yatagawiwa kwa kila kanda nchini, magari haya kila gari linakuwa na
mengine 10 ambayo yanakuwa na huduma mbalimbali za kiafya kama chumba
cha upasuaji, store ya madawa, maji na mengine ambayo yanahitajika kutoa
huduma kwa mgonjwa,” alisema Dk. Kigwangalla.
Naibu
Waziri wa Afya, Ustawi wa Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Hamisi
Kigwangalla na balozi wa Korea nchini, Song Geum-young wakipiga picha ya
pamoja baada ya kumaliza mazungumzo.
Aidha
aliongeza kuwa magari hayo ya kutolea huduma za afya ambayo yanatembea
‘mobile clinic’ yanataraji kuletwa nchini mwakani mwezi Januari na
kwasasa wizara imetakiwa kuandika andiko la mradi ili kuonyesha kuwa
imekubali kuingia katika mradi huo ambao kwa kiasi kikubwa utaweza
kurahisisha upatikanaji wa huduma za kiafya kwa maeneo ambayo yana vituo
vichache vya afya.
Na Rabi Hume, MO Blog
Katibu
wa Balozi wa Korea, Songwon Shin akibadilishana mawasiliano na Naibu
Waziri wa Afya, Ustawi wa Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Hamisi
Kigwangalla katikati ni balozi wa Korea nchini, Song Geum-young.
Naibu
Waziri wa Afya, Ustawi wa Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Hamisi
Kigwangalla akiagana na balozi wa Korea nchini, Song Geum-young baada ya
kumaliza kufanya mazungumzo.






0 maoni:
Chapisha Maoni