Jumanne, 5 Julai 2016

Tanzania, Uganda zajadili utekelezaji wa Bomba la Mafuta

 indexKatibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Prof. Justin Ntalikwa wa kwanza kulia, akifuatiwa na Kamishna Msaidizi anayeshughulikia masuala ya Petroli Mwanamani Kidaya (katikati) na Mratibu wa Mradi, Salum Mnuna (kushoto) wakifuatilia majadiliano wakati wa kikao cha  Makatibu Wakuu wa nchi za Uganda na Tanzania, kilichohusu utekelezaji wa Mradi wa bomba la Mafuta ghafi kutoka Hoima nchini Uganda hadi Bandari ya Tanga, Tanzania.
Kikao hicho kilifanyika tarehe 04.07.2016, kabla ya kikao cha Mawaziri wan chi husika. Aidha, Wataalam wengine (hawapo pichani) waliohudhuria kikao hicho kwa upande wa Tanzania walitoka Wizara ya Nishati na Madini, Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) na Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA).
Pia, kwa upande wa Uganda waliwakilishwa na Wizara ya Nishati na Maendeleo ya Madini, wadau wa sekta hizo kutoka idara mbali mbali za Serikali na wawekezaji kampuni za Total, CNOOC na Tullow.
Vikao hivyo ni sehemu ya Maandalizi ya ripoti iliyowasilishwa katika kikao cha Mawaziri cha tarehe 5.07.201, Hoima nchini Uganda.
BWaziri wa Nishati na Madini (katikati mstari wa kwanza kulia) akiongoza Wataalam wa Watanzania katika kikao cha Mawaziri wa  Tanzania na Uganda kujadili utekelezaji wa Mradi wa bomba la Mafuta kutoka Hoima nchini Uganda hadi Bandari ya Tanga. Kikao cha Mawaziri kimefanyika tarehe 5.07.2016.

0 maoni:

Chapisha Maoni