Posted by Esta Malibiche on Nov4,2016 in NEWS
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimsikiliza Mtangazaji Tido Mhando
wakati akiuliza maswali kutoka kwa wahariri wa vyombo mbalimbali
aliokutana nao kwa mahojiano leo Ijumaa Oktoba 4, 2016 katika ukumbi w3a
mikutano wa Ikulu jijini Dar es salaam
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe
Magufuli akimsikiliza Msanii Mrisho Mpoto akiimbwa wimbo wa “SIJONZE”
wakati alipokutana na wahariri kwa mahojiano leo Ijumaa Oktoba 4, 2016
katika ukumbi w3a mikutano wa Ikulu jijini Dar es salaam
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimsikiliza Mkurugenzi Mkuu wa Shirika
la Utangazaji la Taifa (TBC) Dkt. Ayoub Rioba wakati wa kupokea maswali
kutoka kwa wahariri wa vyombo mbalimbali aliokutana nao kwa mahojiano
leo Ijumaa Oktoba 4, 2016 katika ukumbi wa mikutano wa Ikulu jijini Dar
es salaam
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akijibu maswali
kutoka kwa
wahariri wa vyombo mbalimbali aliokutana nao kwa mahojiano leo Ijumaa
Oktoba 4, 2016 katika ukumbi wa mikutano wa Ikulu jijini Dar es salaam
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimsikiliza mwanahabari Sammy Awami wa
BBC wakati akiuliza maswali kutoka kwa wahariri wa vyombo mbalimbali
aliokutana nao kwa mahojiano leo Ijumaa Oktoba 4, 2016 katika ukumbi w3a
mikutano wa Ikulu jijini Dar es salaam
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimsikiliza Mhariri Mtendaji wa
magazeti ya Serikali (TSN) Dkt. Jim Yonazi wakati akiuliza maswali
kutoka kwa wahariri wa vyombo mbalimbali aliokutana nao kwa mahojiano
leo Ijumaa Oktoba 4, 2016 katika ukumbi w3a mikutano wa Ikulu jijini Dar
es salaam
………………………………………………………………………
Na Beatrice Lyimo-MAELEZO-Dar es Salaam.
RAIS
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amewataka
waandishi wa habari nchini kutotumika kama mgongo kwa baadhi ya wamiliki
wa vyombo vya habari katika kupinga muswada wa sheria wa huduma za
habari wa mwaka 2016.
Aliyasema
hayo leo Jijini Dar es Saalam wakati wa mkutano wake na Wahariri wa
vyombo vya habari nchini katika kuhadhimisha mwaka mmoja wa Utawala
wake, ambapo alisema kuwa kumekuwa na baadhi ya wamiliki wenye mashali
binafsi katika kupinga mchakato mzima wa upatikanaji wa Sheria ya Huduma
za Habari nchini.
“mchakato
wa kupata Sheria ya huduma za habari umechelewa kutokana na sababu
mbalimbali hivyo ninawataka wanahabari kutozungumza kwa mgongo wa
wamiliki mbalimbali wenye maslahi binafsi katika kupinga upatikanaji wa Sheria hiyo.
Alisema
kuwa suala la Muswada wa Huduma za Habari upo mikononi mwa wabunge
ikiwa ni muhimili unaojitegemea na hatoweza kuingilia maamuzi ya bunge
na kuacha wabunge kutimiza wajibu wao katika utungaji na upatikanaji wa
Sheria hiyo.
Aidha,
Rais Magufuli alisema kuwa anafahamu baadhi ya changamoto zilizopo kwa
waandishi wa habari hasa katika masuala ya maslahi hivyo muswada huo
utasaidia katika kutatua changamoto hizo na pia utaifanya tasnia ya
habari kuwa taaluma itakayoheshimika kama taaluma nyingine.
0 maoni:
Chapisha Maoni