Posted by Esta Malibiche on Nov 7,2016 in MICHEZO
Zile mechi tatu za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara za raundi ya Nane Duru la Kwanza, sasa zitafanyika Jumatano.
Michezo hiyo inahusisha timu za
Mwadui ya Shinyanga na Azam FC ambayo ilipewa jina la Mechi Na. 57
itachezwa Uwanja wa CCM Kambarage wakati Simba itasafiri hadi Mbeya
kucheza na Tanzania Prisons katika mchezon Na. 60 Uwanja wa Kumbukumbu
ya Sokoine ilihali Young Africans ya Dar es Salaam itakuwa mwenyeji wa
Ruvu Shooting Uwanja wa Uhuru jijini katika mchezo Na.59.
Mechi zilipangiwa ratiba, lakini
tarehe zake hazikupangwa (TBA). Tayari Bodi ya Ligi Kuu ya Vodacom
(VPL), imewasiliana na wahusika kuhusu mabadiliko hayo. Sababu ya kuvuta
nyuma michezo hiyo ni kutoa nafasi ya maandalizi ya kambi ya timu ya
Tanzania ‘Taifa Stars’ inayotarajiwa kusafiri Ijumaa wiki hii kwenda
Harare Zimbabwe kwenye mchezo wa kirafiki wa kimataifa unaotarajiwa
kufanyika Novemba 13, maka huu.
0 maoni:
Chapisha Maoni