Posted by Esta Malibiche on Nov 3,2016 in TECHNOLOJIA
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi
na Umeme TEMESA Dkt Mussa Mgwatu (kushoto) akiongea na Meneja wa TEMESA
Mtwara Mhandisi Said Mongomongo alipotembelea ofisi hiyo, ili kujionea
hali halisi ya kituo hicho pamoja na utendaji kazi wake.
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi
na Umeme TEMESA Dkt Mussa Mgwatu (kulia) akisikiliza malalamiko ya
abiria wa MV. Mafanikioalifanya ziara Mkoani Mtwara.
Kivuko cha MV. Kilambo kinachotoa
huduma ya uvushaji katika Mto Ruvuma, unaozitenganisha nchi za Msumbiji
na Tanzania katika eneo la KIlambo (TANZANIA) na Namoto (Msumbiji). .
Kivuko hiki kinasimamiwa na Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA)
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi
na Umeme ( TEMESA) Dkt Mussa Mgwatu akikagua kitabu kinachoonyesha
taarifa za safari zinazofanywa na kivuko pamoja na hali ya kivuko
kinapokuwa safarini.
Picha zote na Theresia Mwami TEMESA Mtwara.
…………………………………………….
Na Theresia Mwami TEMESA Mtwara.
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi
na Umeme (TEMESA) Dkt. Mussa Mgwatu amesema kuwa hajaridhishwa na
ukusanyaji wa mapato na madeni katika kituo cha Mtwara katika robo ya
kwanza ya mwaka wa fedha 2016/2017 ambapo karakana imekusanya asilimia
20% tu ya kiasi cha pesa ilichozalisha.
Dkt Mgwatu amesema kuwa
hatovumilia uzembe wowote utakaojitokeza katika suala la ukusanyaji wa
mapato na madeni katika vituo vyote vya TEMESA nchini.
“Hatuwezi kuendesha vituo na
karakana zetu kwa mwendo huu hivyo inatupasa kuongeza juhudi katika
kufuatilia madeni” alisema Dkt. Mgwatu.
Kwa upande wake Meneja wa TEMESA
Mtwara Mhandisi Said Mongomongo amesema kuwa kuna changamoto za Taasisi
nyingi kutolipa kwa wakati gharama za matengenezo ya magari na mashine
mbalimbali katika karakana yake.
Mhandisi Mongomongo amewataja
baadhi ya wadaiwa sugu kuwa ni pamoja na Shirika la Umeme Tanzania
(TANESCO) na Ofisi ya Katibu Tawala mkoani Mtwara.
Akiwa mkoani Mtwara, Dkt Mgwatu
ametembelea Kivuko cha MV. Mafanikio kinachotoa huduma ya usafiri kati
ya Msangamkuu na Msemo pamoja na Kivuko cha MV. Kilambo kinachotoa
huduma kati ya Kilambo (upande wa Tanzania) na Namoto (upande wa
Msumbiji).
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi
na Umeme (TEMESA) Dkt. Mussa Mgwatu yupo katika ziara ya kikazi katika
mikoa ya Lindi na Mtwara kuangalia utendaji kazi wa vituo hivyo.
0 maoni:
Chapisha Maoni