Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam,
Paul Makonda akizungumza kwenye hafla ya kukabidhiwa madawati yenye
tahamani ya Sh. Milioni 20 yaliyotolewa na shule za Al Murtazir, ikiwa
ni kuunga mkono kampeni ya Mkuu wa Mkoa huyo kuhakikisha watoto wote
wanakaa kwenye madawati leo jijini Dar es Salaam.
Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es
Salaam, Alhad Mussa Salum akizungumza machache kwenye hafla ya kukabidhi
Madawati yenye jumla ya thamani ya milioni 20 yaliyotolewa na shule
za Al Murtazir, ikiwa ni kuunga mkono kampeni ya mkuu wa mkoa huyo
kuhakikisha watoto wote wanakaa kwenye madawati leo jijini Dar es
Salaam.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam,Paul Makonda akikata utepe kwenye hafla ya kukabidhiwa wadawati leo jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa mkoa wa Dar es
salaam,Paul Makonda akikabidhiwa madawati na Mwekiti wa Bodi ya Elimu ya
Shule za Al Murtazir Azim Dewji ili kuunga mkono juhudi za serikali ya
awamu ya tano inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
ambae pia alikuawa mwalimu Mh.John Pombe Mgufuli
Sehemu ya wazazi na wanafunzi wa Shule ya Al-Mutanzil leo jijini Dar es Salaam.Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya Jamiii.
Idadi ya Wataalamu wa Sayansi
imekuwa ikikua kwa kasi kutokana na sekta hiyo kuwa chanzo cha
maendeleo na ugunduzi na kufanya kupata maendeleo.
Hayo yamesemwa na Mkuu na Mkoa
wa Dar es salaam, Paul Makonda wakati wa hafla ya Kukabidhiwa Madawati
yenye thamani ya Sh. milioni 20 kutoka kwa Mwenyekiti wa Bodi ya Elimu
ya Shule za Al Muntazir, Azim Dewj
“Nimeomba sana wazazi
kuhamasisha watoto wao kusoma sayansi, ukifanikiwa kwenye hayo masomo
sio kwamba tu utaajiriwa lakini utaajiriwa sehemu unayoitaka kutokana na
ajira kuwa nyingi ukitofautisha na masomo tuliyosoma sisi,”amesema
Makonda.
Nae Mwenyekiti wa Bodi ya
Elimu ya Shule za Al Muntazir,Azim Dewji amesema ‘’tumeona litakuwa
jambo la busara kama tutaunga mkono juhudi za serikali ya awamu ya tano
tano inayoongozwa na Rais dk. John Pombe Magufuli ambaye pia alikuwa
mwalimu.
0 maoni:
Chapisha Maoni