Mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela akimtwisha Ndoo ya Maji Bi.Theobadina Ngailo Mara baada ya kukabidhi Mradi wa Maji katika kijiji cha Lupalama Jimbo la Kalenga uliogharimu kiasi cha Mill.35 na kufadhiliwa na Shirika la E.P.I.C (Everyday People Initiate Changes) la Marekani
Na Esta
Malibiche
Iringa
Mkuu
wa wilaya ya Iringa Mh Richard Kasesela amezindua mradi wa maji Saafi na salama
katika kijiji cha Lupalama kilichopo katika Tarafa ya kalenga Wilayani
Iringa,uliogharimu kiasi cha Tsh.35 Mill.
Mradi huo umefadhiliwa
na Shirika la E.P.I.C (Everyday People Initiate Changes) la Marekani liloanzishwa
na Mwanamuziki wa Marekani Tinara Moore,ambaye aliwahi kutembelea Tanzania na
baadae kuamua kutoa misaada mbalimbli.
Akikabidhi Mradi
huo kwa wanakijiji wa lupalama mkuu wa wilaya ya Iringa amewaomba wana kijiji hao kuusimamia vema mradi huo
kwani Ofisi yake ina mpango wa kuhakikisha maji hayo yana sambazwa katika
Maeneo Yote ya kijiji hicho ili kuhakikisha upatikanaji wa maji kwa wingi.
‘’’’’’Matumaini yangu kuona Maji haya yana wafikia wanakijiji
wote wa lupalama ikibidi na maeneo ya Jirani wapate pia maji haya nitoe agizo
kwa serikali ya kijiji kuunda kamati ya kusimamia na kutunza mradi huu ili
uendelee kufanya kazi na kunufaisha wengi wakati mimi niki hangaika kuona jinsi
gani tunapata pampu ya Umeme ikishindikana hata ya kutumia nguvu ya jua ili
tusambaze maji haya sehemu nyingi zaidi”Alisema Kasesela
Katika hotuba
yake Mkuu wa wilaya alihimiza wananchi kutumia vizuri chakula,kutokana na mvua
kuchelewa kunyesha ili waweze kuepuka na baa la njaa,pia aliwasihi mara mvua
zitakapoanza kunyesha wqatumie muda huo katika kilimo na wajitahidi kupanda
mazao ya muda mfupiyatakayoweza kukomaa haraka na kuvunwa.
Mvua mwaka huu sio za kuridhisha hivyo basi
ipo hofu ya kukosekana chakula ni muhimu wananchi wakatunza chakula na kulima
mazao yenye kuhimili ukamE’’’’’Alisema Kasesela
Aidha Dc
Kasesela aliiagiza Serikali ya kijiji Kuanza mara moja Mchakato wa ujenzi wa
kituo cha afya kijijini hapo kwani ni kero ya muda mrefu hasa kwa akina mama
kwani wana lazimika kutembea kilomita saba kufuata huduma ya afya
“Nawaombeni Zoezi hili lianze mapema sana na ikibidi kila
mwanakijiji ashiriki kukusanya mawe ya ujenzi na pindi mkiwa tayali ujenzi
uanze mara moja”.Alisema Kasesela
Akizungumza
wakati wa kukabidhi mradi huo Muwakilishi wa E.P.I.C Tanzania Bwana Johnson
Mkini Kisinda alisema kuwa mradi huo umeghalimu pesa zaidi ya milioni therasini
na tano hadi kukamilika .
‘’’’’ “Hiki ni
kisima cha pili kwa urefu katika visima vyote tulivyo chimba kwani Lengo
lilikuwa kuchimba mita sabini tu ila tulikosa maji tukalazimika kuchimba mita
mia moja na themanini kwenda chini hadi kuyafikia maji.
Kisinda
aliwataka wanakijiji wa Lupalama kuwa walinzi wa miundo mbinu hiyo ya maji
kwani ni kwa faida yao wenyewe.
Theobadina
Ngailo ni mwanakijiji mkazi wa Lupalama
akizungumza kwa niaba ya wanakijiji alisema kuwa kwa muda mrefu walikuwa
wanakabiliwa na changamoto ya kutembea umbali mrefu kutafuta maji,na kushindwa
kufanya shughuli za maendeleo kwasababu ya maji,hivyo alilishukuru shirika la E.P.I.C kwa kutatua changamoto hiyo
‘’’’’’’Tulikuwa tukilazimika kutembea saa zima
kufata maji mtoni nabado maji haya kuwa ya uhakika kwa maana kipindi cha
kiangazi mto ulikuwa una kauka jambo lililopelekea kupata shida kubwa sana
katika upatikanaji wa maji. Tulikuwa tunatumia hata maji ya kwenye vidimbwi
ambayo sio salama kwa matumizi ya binadamu kwani muda mungine tulikuwa
tukichangia maji hayo na mifugo jambo lilipolekea kulipuka kwa magonjwa kama
kuhara”.” ‘’’’Alisema Theobadina
|
0 maoni:
Chapisha Maoni