Katibu
wa BAKWATA mkoa wa Singida, Burhan Mlau, akitoa nasaha zake kwenye
hafla ya futari iliyoandaliwa na mwenyekiti CCM mkoa, Martha Mlata
kufutarisha baadi ya waumini wa dini ya kiislamu mkoani hapa. Wa tatu
kulia ni Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchema aliyekuwa mgeni rasmi
katika hafla hiyo ya futari. Wa pili kushoto ni mkuu wa mkoa wa Singida,
Mhandisi Mathew Mtigumwe na wa kwanza kushoto ni mkuu wa wilaya ya
Ikungi, Miraji Mtatu. Kulia ni Mwenyekiti wa CCM mkoa, Martha Mlata.
Mwenyekiti
wa CCM mkoa wa Singida, Martha Mlata, akitoa shukrani zake kwa waumini
wa dini ya kiisalamu kuitikia wito wake kushiriki pamoja futari jioni ya
juzi. Wa tatu kushoto waliokaa ni Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu
Nchemba, wa pili kushoto ni mkuu wa mkoa wa Singida, Mhandisi Mathew
Mtigumwe na wa kushoto ni mkuu wa wilaya ya Ikungi, Miraji Mtatur.
Aliyesimama ni Katibu Mkoa wa Singida BAKWATA, Alhaj Burhan Mlau.
Waziri
wa Mambo ya Ndani na mbunge wa jimbo la Iramba Magharibi,
Mwigulu,akizungumza kwenye hafla ya futari iliyoandaliwa na mwenyekiti
wa CCM mkoa wa Singida. Wa pili kushoto ni mkuu wa mkoa wa Singida,
Mhandisi Mathew Mtigumwe na wa kwanza kushoto ni mkuu wa wilaya ya
Ikungi, wakati kulia ni mwenyekiti wa CCM na mbunge wa viti maalum mkoa
wa Singida, Martha Mlata.
Mkuu
wa wilaya ya Ikungi mkoa wa Singida, Miraji Mtaturu, akichukua futari
iliyoandaliwa na mwenyekiti CCM na mbunge wa viti maalum mkoa wa
Singida, Martha Mlata.
Mkuu
wa mkoa wa Singida, Mhandisi Mathew Mtigumwe, akichukua futari
iliyoandaliwa na mwenyekiti CCM na mbunge wa viti maalum mkoa wa
Singida, Martha Mlata. Anayeangalizana na kamera ni Waziri waMambo ya
Ndani, Mwigulu Nchemba.
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Singida, Martha Mlata, akimpongeza kijana aliyekuwa akitoa dua. (Picha na Nathaniel Limu)
Waziri
wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba, amesema kuwa serikali imejipanga
vizuri kuhakikisha taratibu, ratiba na maadhimisho muhimu ya madhehebu
ya dini nchini, yanafanyika bila kuvurugwa na baadhi ya watu mwenye nia
mbovu.
Mwigulu
ambaye pia ni mbunge Jimbo la Iramba Magharibi, aliyasema hayo kwenye
hafla ya kufuturisha baada ya viongozi na wananchi wa dhehebu la
kiislamu kutoka wilaya zote za mkoa wa Singida. Futari hiyo iliandaliwa
na mwenyekiti wa CCM mkoa na mbunge wa viti maalum, Martha Mlata.
Alisema
madhehebu ya dini nchini yameendelea kuiwezesha Tanzania iendelee
kudumisha amani na utulivu hivyo ni wajibu wa serikali kuyaimarishia
ulinzi ili wananchi wake wazidi kupata mafundisho ambayo yatasaidia
wananchi wenye nia mbaya wanabadilika na kuwa watu wema.
“Kutokana
na mchango huo ambao pamoja na faida zake nyingi ikiwemo wananchi
kujiletea maendeleo yao kwa uhuru mpana, sisi wa wizara ya mambo ya
ndani, hatukubali ustawi wa madhehebu ya dini uchafuliwe kwa namna
yoyote ile”,alisisitiza.
Alisisitiza
zaidi, Mwigulu alisema waumini wa dini ya kiislamu wasiwe na hofu wala
wasi wasi wowote, kuelekea siku kuu ya Iddi Elftiri na kwamba
wataisherehekea bila usumbufu wa aina yo yote.
“Hata
ndugu zetu wanaotarajia kwenda kuhiji mwaka huu, wasiwe na hofu yoyote,
tutahakikisha hakuna mtu au kikundi cha watu kitakachochafua taratibu
zao za kwenda kutimiza nguzo muhimu za dhehebu lao la dini,” alisema
Mwigulu.
Kwa
upande wake, Mlata alisema ameandaa hafla hiyo ya futari baada ya
kusukumwa na imani kwamba Watanzania siku zote, niwa ni wamoja
hawabaguliwi na itikadi ya kisiasa wala kwa dini zao.
“Kila Mtanzania anaheshimu imani
ya dini ya mwenzake. Kitendo hiki kina mchango mkubwa sana kwenye amani
na utulivu wetu, na ndio maana nchi yetu imeendelea kuwa kisiwa cha
amani,” alisema mwenyekiti huyo.
Mlata
ambaye ni mwimbaji mahiri nchini wa nyimbo za kwaya, pia alitoa msaada
wa vitabu vipya vya quran 100 na maboksi matano ya tende.






0 maoni:
Chapisha Maoni