Wafanyakazi
wa kampuni ya TBL Group wamepongeza hatua ya kampuni kutekeleza mpango
wa Afya kwanza ambao unawawezesha kujua hali ya afya zao wakiwa
kazini,kujengewa mazingira ya kufanya mazoezi na familia zao na kupatiwa
ushauri wa jinsi gani ya kukabiliana na changamoto za magonjwa ambayo
yamekuwa yakiongezeka kwa kasi nchini.
Wakiongea
baada ya kumaliza kushiriki mbio za kilometa 5 zilizotayarishwa na
taasisi ya Ocean Church na kufanyika jijini Dar es Salaam baadhi yao
walisema kuwa utaratibu huu ni wa muhimu wa kuwawezesha kushiriki katika
mazoezi kwa ajili ya kuweka afya zao na familia zao vizuri.
Akiongea kwa niaba ya
wafanyakazi wenzake baada ya kumalizika zoezi hilo la utekelezaji wa
progamu ya Afya Kwanza Sam Mhagama kutoka TBL Ilala alisema kuwa mpango
huu ni mzuri kwa kuwa unawawezesha wafanyakazi kujenga utamaduni wa
kupima afya zao mara kwa mara,kupata ushauri wa kitaalamu na kufanya
mazoezi ili kuimarisha afya zao.
Kwa
upande wake Seleman Mbena alisema kuwa utaratibu wa kusogeza huduma za
afya sehemu za kazi na kufanya mazoezi ni mzuri kwa kuwa unawawezesha
wafanyakazi kupata elimu ya kujikinga na maradhi mbalimbali na wale
wanaosumbuliwa na maradhi wanapata elimu ya jinsi ya kukabiliana nayo
pia wanapata elimu ya lishe bora na jinsi ya kukabiliana na changamoto
ya magonjwa hasa yanayosababishwa na maisha ya kisasa wanayoishi
wafanyakazi wengi.
Mratibu wa Programu ya Afya
Bora wa kampuni ya TBL Group, Julieth Mgani alisema Japo suala la afya
limekuwa halipewi kipaumbele na waajiri wengi nchini lakini ni suala
muhimu la kuzingatiwa na waajiri wengi ili kuleta tija na ufanisi, kwa
kuwa wafanyakazi wenye afya bora wanashiriki vizuri katika shughuli za
uzalishajiAlisema Afya Bora kwa wafanyakazi haina maana wafanyakazi kulipiwa gharama za matibabu mahospitalini na waajiri wao bali inahusisha mambo mengi kuhusiana na afya zao na afya za familia zao.
Mgani
alisema Alisema katika sehemu za kazi suala la Afya linapaswa
kuzingatiwa wakati wote sio kulipa kipaumbele mara chache wakati wa
kuadhimisha siku ya Afya au ya ugonjwa fulani kama ambavyo imekuwa
mazoea kufanyika na siku hiyo ikipita hakuna kinachoendelea.
Baadhi ya wafanyakazi wa TBL Group wakionyesha medali zao muda mfupi baada ya kumalizika kwa matembezi.
Baadhi
ya wafanyakazi wa TBL Group na familia zao katika picha ya pamoja muda
mfupi baada ya kumalizika kwa matembezi yaliyotayarishwa na taasisi ya
Ocean Church.
0 maoni:
Chapisha Maoni