Kamishina
wa biashara wa umoja wa ulaya Cecilia Malmström amesema Uingereza
inaweza kuanza majadiliano ya mikataba mipya ya kibiashara iwapo tu
itakuwa imejitoa kabisa katika umoja huo.
Katika mahojiano na BBC amesema kuna aina mbili za majadiliano ya utekelezaji wa makubaliano hayo.
"Uhusiano kati yetu na uingereza kwa siku zijazo hautajadiliwa chini ya kifungu cha 50,ambacho ndicho kigezo cha kujitoa.
Hivyo kuna aina mbili tu za majadiliano,moja unajitoa,kisha unajadiliana namna mpya ya uhusiano,au vyovyote inavyokuwa"
Bi.Malmstrom
ameongeza kuwa mpaka mikataba hiyo isainiwe ndipo biashara inaweza
kufanyika chini ya taasisi ya kimataifa ya kibiashara.
|
0 maoni:
Chapisha Maoni