Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Dkt.
Augustine Mahiga (kulia) akizungumza na Waziri wa Mambo ya Nje wa
Jamhuri ya Rwanda, Mhe.Loiuse Mushikiwabo, alipomtembelea leo katika
Ofisi za Wizara Jijini Dar es Salaam. Mazungumzo yao yalijikita katika
kuimarisha na kuboresha mahusiano yaliyopo baina ya nchi hizo mbili,
pamoja na Ziara ya Rais wa Jamhuri ya Rwanda Mhe. Paul Kagame
anayetarajiwa kuwasili nchini kesho kwa ziara ya siku mbili.
Kaimu
Mkuu wa Itifaki katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika
Mashariki, Bw. James Bwana alipokuwa akimkaribisha Mhe. Waziri
Mushikiwabo mara baada ya kuwasili Wizarani.
Kutoka
kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya Afrika katika Wizara ya Mambo ya Nje
na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Samuel Shelukindo, akiwa
na Kaimu Mkuu wa Itifaki, Bw. James Bwana na Afisa Mambo ya Nje, Bw.
Medard Ngaiza wakifuatilia mazungumzo.
Balozi
wa Jamhuri ya Rwanda nchini, Mhe. Eugene Kayihura (kulia) pamoja na
Afisa aliyeambatana na Mhe. Waziri Mushikiwabo wakifuatilia mazungumzo.
Wakati mazungumzo yakiendelea.
Wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya mazungumzo.
0 maoni:
Chapisha Maoni