Mhandisi
wa mitambo wa Studio za Bunge Bi. Upendo Mbele akitoa maelezo kwa
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Mstaafu Damian Lubuva (wa
kwanza kulia) na Ujumbe wake juu ya namna wanavyotekeleza majukumu ya
kurusha vipindi kwa kuzingatia sheria na Kanuni za Bunge wakati wa Ziara
iliyolenga kukabidhi ripoti ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015.
Mwenyekiti
wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Mstaafu Damian Lubuva (wa kwanza
kushoto) akifuatilia Kikao cha Bunge mapema Jana wakati wa ziara ya Tume
hiyo Bungeni Mjini Dodoma kabla ya kuahirishwa kwa Mkutano wa tatu wa
Bunge la kumi na moja .
Kamishna
wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Prof. Amon Chaligha akiwa ndani ya Maktaba
ya Bunge wakati wa Ziara ya Tume hiyo Bungeni Mjini Dodoma.
Mkurugenzi
wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano Ofisi ya Bunge Bw. Didas Wambura
(wa kwanza kulia) akitoa maelezo kwa Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya
Uchaguzi Jaji Mstaafu Damian Lubuva (hayupo pichani) na Ujumbe wake
wakati wa ziara ya Tume hiyo Bungeni Mjini Dodoma.
(Picha na Frank Mvungi-Dodoma)
0 maoni:
Chapisha Maoni