08:30
Ashraph
Omary (wa pili kushoto) akizungumza jambo kwa niaba ya
Wanachama/Wafanyakazi kutoka Taasisi ya METDO (Mining and Environmental
Transformation For Development Organisation, walipotembelea Kituo cha
Wazee Bukumbi kilichopo Misungwi mkoani Mwanza.
Wafanyakazi
wa METDO wakiambatana na Mwenyekiti wa Chama cha Madereva wa daladala
Kanda ya Ziwa, Hassan Dede pamoja na Wanafunzi wa Geita International
School, waliwakabidhi wazee wanaolelewa katika kituo hicho msaada wa
mahitaji mbalimbali ikiwemo chakula.
Taasisi ya METDO kupitia kwa msemaji wake, Ashraph Omary, iliwahimiza
wanajamii kwa kushirikiana na taasisi za serikali na binafsi kuwasaidia
wazee wanaoishi katika kituo hicho ili kuondokana na changamoto
zinazowakabiri ikiwemo ukosefu wa mavazi, chakula, matibabu pamoja na
ujenzi wa uzio kituoni hapo ikiwa ni miongoni mwa changamoto
zilizoanishwa kuwakabiri wazee hao.
0 maoni:
Chapisha Maoni