Jeshi la Uganda katika msafara wa kijeshi likielekea Juba, Julai 14, 2016.
Hali ya
usalama bado ni ya wasiwasi nchini Sudan Kusini licha ya hali ya utulivu
kurejea, baada ya mapigano ya mwishoni mwa wiki iliyopita. Hakuna
mapigano Alhamisi hii Julai 14 kwa siku ya tatu mfululizo.
Lakini
nchi nyingi za kigeni zimeendelea kuwarejesha nyumbani raia wao. Na
Alhamisi hii asubuhi, msafara wa majeshi ya Uganda umeingia katika ardhi
ya Sudan Kusini, ukiwa na sababu rasmi, kuwarejesha nyumbani raia wa
Uganda.
Askari
zaidi ya mia moja na malori hamsini kutoka Uganda wameingiakatika ardhi
ya Sudan Kusini Alhamisi hii Julai 14. Hatua hiyo ilitangazwa siku moja
kabla, na msafara ulichelewa kutokana na uamuzi wa Serikali ya Sudan
Kusini kufunga mipaka yake.
"Vikosi
vyetu vya vya jeshi viko njiani vikieleea katika mji wa Nisitu, kilomita
30 ana mji wa Juba. Hatuna nia ya kwenda mbali zaidi ya mji wa Nisitu,
wala nia ya kwenda hadi katika mji wa Juba.
Tayari kuna raia 2,000 wawa
Uganda ambo wanasubiri kurejeshwa nyumbani.
Tunaamini kwamba operesheni
hii itadumu siku 10, hadi 20, "amesema msemaji wa serikali ya Uganda.
Kuhusu
muda wa operesheni, kumekua na hisia tofauti. Afisa wa Idara ya Ujasusi
ya Uganda amelielezea shirika la habari la AFP kwamba vikosi vya jeshi
la Uganda vnaweza kukaa muda mrefu kuliko ilivyotarajiwa mjini Juba, na
kuongeza, "tumefanya hivyo katika siku za nyuma, kwa nini tusifanyi
hivyo kwa sasa? "
0 maoni:
Chapisha Maoni