…………………………………
SHIRILA
la ugavi wa umeme Tanesco Mkoa wa Pwani limefanikiwa kumkamata moja ya
mteja wake ambaye ni mmiliki wa yadi ya magari ya White star iliyopo
kiluvya kwa Komba nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam kwa kosa la
kuhujumu miundombini kwa kufanya wizi baada ya kuamua kujiunganishia
umeme kinyemela wa njia tatu kinyume na taratibu na sheria za nchi.
Mteja
huyo alikamata baada ya kufanyika kwa msako mkali kwa wateja ambao
wanaiba umeme na kuweza kubaini katika yadi hiyo kuna hujuma ambayo
imefanyika ya kujiunganishia umeme bila ya kufuata taratibu zozote za
Tanesco.
Akizungumza
katika eneo hilo la tukio Afisa Usalama wa Tanesco Mkoa wa Pwani Henry
Byarugaba alisema kwamba baada ya kufanya ukaguzi waliweza kukuta mtaja
huyo alijulikana kwa jina la Munila Mbowe ambapo aliweza kukamatwa na
kupelekwa katika kituo cha polisi cha Kibaha.
Byarugaba
alisema kwamba mteja huyo alikuwa anatumia umeme wa wizi kutokana na
kujiunganishia laini tatu za nyaya ambapo kutokana na wizi huo ameseza
kulisababishia hasara shirika zaidi ya shilingi milioni 50.
“Kama
mnavyoona ndugu waandishi katika kufanya msako wetu wa kawaida tumeweza
kumkamata mmiliki wa yadi ya magari ya white star ambayo ipo kiluvya
kwa kombo kwa kosa la kuiba umemembila ya kuzingatia sheria zozote na
kwamba ameweza kujiunganishia njia tatu ambazo zilikuwa zinapitisha
umeme kwa matumizi ambayo sio sahihi katika eneo hilo,”alisema
Byarugaba.
Aidha
Byarugaba alisema mteja huyo amekuwa akifanya vitendo vya kuhujumu
miundombinu yao na kufanya uharibufu mkubwa hali ambayo inaweza kuleta
madhara makubwa ya kutokea kwa majanga ya moto kutokana na
kujiunganishia umeme bila ya kuwatumia wafanyakazi wa shirikika la
umemem Tanesco.
Pia
alisema kuwa mteja huyo amekuwa ni sugu kwa kipindi cha muda mrefu
kutokana na kujirudia kwa makosa kama hayo kwani mwaka jana wakati
wanafanya msako kwa wateja wao wanaohujumu miundombinu waliweza kumkuta
akiiba tena umeme na walimpeleka polisi na hatua kali za kisheria
ikiwemo kumlipisha faini.
“Jamani
ndugu waandishi huyo mteja wetu ambaye anajulikana kwa jina la Munira
Mbowe amekuwa akifanya matukio haya kwa kipindi cha muda mrefu na
kutokana na hali hii amelitia hasara shirika la umeme, maana mwaka jana
tulimkamata tena akiifanya vitendo kama hivi na tulimfukisha katika
vyombo vya sheria lakini nashangaa amekuja na staili hyingine ya wizi
kwa kutumi tena njia tatu za umeme hii ni hatari sana.
Kwa
upande wake mmoja ya wamilii ya yadi hiyo ya Munira Mbowe alipoulizwa
na waandishi wa habari kuhusina na tumuma za wizi huo alisema kwamba
yeye afahamu lolote juu ya suala hilo kwani mara nyingi yeye anafanyia
shughuli zake jijini Dar es Salaam.
“Ni
kweli tumekutwa na kosa na kuiba umeme lakini jamani waandishi nataka
niwaeleze kuwa mimi siusiki na kingine nawaomba msinitoe katika vyombo
vya habari kwani haya ni maisha tu, sio vizuri kunitoa jamani mimi
sihusiki kabisa katika wizi huu labda anaweza kuwa ni mlinzi amefanya
hivyo au mume wangu amenificha maana wanaume ni wasiri sana,”alijitetea
Munira.
Kwa
upande wake Kaimu Meneja wa Taneso Mkoa wa Pwani Selemani Mgwila
alisema kwamba kitendo alichokifanya mteja wao ni kosa kubwa sana kwani
umeme waliokuwa wanatumia katika yadi hiyo ulikuwa unapotea bure na
kusababisha upotevu mkubwa wa mapato.
Aidha
Mgwila aliwaomba wananchi wote wa Mkoa wa Pwani kuepukana na watu ambao
wanajifanya ni watumishi halali wa tanesco na endapo wakiwabaini
wahakikishe wanatoa taarifa mapema kwa vyombo vya dola ili waweze
kuchukuiliwa hatua kali za kesheria kwani baadhi yao ni matapeli.
SHIRIKA
la umeme Tanesco Mkoa wa Pwani limekuwa likiingia hasara kubwa kutokana
na baadhi ya wateja wake kuamua kujiunganishia umeme kinyemela pasipo
kuzingatia sheria na taratibu na wakati mwingine kupelekea kutokea kwa
majanga ya moto.
0 maoni:
Chapisha Maoni