Mwenge
wa Uhuru ukiwasili kwenye uwanja wa mpira wa Mchinga I,wilaya ya Lindi
vijijini ambapo ulizindua miradi mbalimbali ya kimaendeleo katika
Majimbo mawili wa wilaya hiyo, jimbo la Mchinga na jimbo la Mtama.
Viongozi mbali mbali wakiwa wamesimama tayari kuupokea Mwenge wa Uhuru katika wilaya ya Lindi Vijijini
Mkimbiza Mwenge wa Uhuru Bw. George Jackson kitaifa akizindua mradi wa maji katika shule ya msingi Mchinga I.
Mbunge
wa Jimbo la Mtama ambaye pia ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na
Michezo Mhe. Nape Nnauye pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Lindi Mhe. Yahaya
Nawanda wakiwaongoza waongoza Mwenge wa Uhuru kitaifa kupita juu ya
daraja lililofunguliwa rasmi na kiongozi wa mbio za Mwenge kitaifa,
Daraja hili linawaunganisha wakazi wa Mchinga II na Mchinga I.
Wanafunzi
wa shule ya sekondari ya kata ya Mnonela wakihushuhudia Mwenge wa Uhuru
kwa kuushika ulipowasili shuleni hapo jimbo la Mtama , Lindi Vijijini.
Mbunge
wa Jimbo la Mtama ambaye pia ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na
Michezo Mhe. Nape Nnauye (kushoto) , mkimbiza Mwenge Kitaifa na Mkuu wa
Wilaya ya Lindi Mhe. Yahaya Nawanda wakiwa wamekalia moja ya madawati 50
yaliokabidhiwa kwa Mwalimu Mkuu wa Shule ya msingi Mnolela.
Mbunge
wa Jimbo la Mtama ambaye pia ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na
Michezo Mhe. Nape Nnauye akitoa heshima kwa Mwenge wa Uhuru kwenye
viwanja vya shule ya msingi Madangwa.
Mbunge
wa Jimbo la Mtama ambaye pia ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na
Michezo Mhe. Nape Nnauye akihutubia wakazi wa Madangwa waliojitokeza
kwenye mkesha wa Mwenge wa Uhuru ambapo aliwaambia kuwa utekelezaji wa
yale aliyoahidi umeanza na kuwahakikishia wananchi wa jimbo lake ahadi
zake zitakamilika mapema zaidi.
BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI
BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI
0 maoni:
Chapisha Maoni