Jumanne, 31 Mei 2016

WAMILIKI WA VYOMBO VYA HABARI NCHINI WATAKIWA KUTOA MIKATABA YA AJIRA KWA WANDISHI WA HABARI



Katibu mkuu wa wizara ya  Habari, sanaa, utamaduni na michezo Prof.Elisante ole Gabriel amewataka waajiri  na wamiliki wa vyombo vya habari nchini kuhakikisha wanatoa mikataba YA AJIRA  kwa waajiliwa wao ili kuleta ufanisi kwa wandishi wa habari
Kauli hiyo ameitoa  jana katika ofisi ya mkuu wa mkoa wa Iringa alipokuwa akizungumza katika kikao kilichowakutanisha wandishi wa habari wa mkoa wa Iringa , wadau wa habari, sanaa,utamaduni na michezo mkoani hapa katika moja ya  ziara yake aliyoifanya jana.
Alisema kumekuwa na changamoto kubwa ya wamiliki wa vyombo vya habari nchini kutotoa mikataba kwa wafanyakazi,kwa kutowapa mikataba ya ajira  itakayowawezesha kuwalipa mishahara  na wengine kuwatumikisha kwa kuwalipa posho tu hali inayopelekea wandishi waliowengi kushindwa kufanya kazi kiufasaha.
‘’’’’’’Sekta ya habari imejidhatiti kuhakikisha Taifa linahabarika kwa habari zilizosahihi na siyo vinginevyo.Hivyo ninawaomba waajili na wamiliki wa vyombo vya habari wahakikishe wanatoa ajira kwa wafanyakazi wao kwa kuwapa mikataba ya kazi na kuwalipa mishahara stahiki ili waweze kuepuka na na rushwa ya bahasha’’’alisema
‘’’’Endapo mwandishi atalipwa vizuri na mwajili wake,ataweza kufanya kazi kwa ufanisi na ufasaha pia ataweza kujiepusha na kununuliwa na mtoa habari kwa kutaka taarifa itolewe kwa matakwa yake yeye.Hivyo waajili hakikisheni mnbawapa mikataba wandishi wenu na mishahara ili waewze kufanya kazi kwa bidii na kufuata kanuni na taratibu za uandishi’’alisema
Prof.Gabriel aliwataka wandishi wahabari  kuepuka matatizo yasiyo ya lazima kwa kuandika habari za uchochezi ambazo zinazonaweza leta mtafaruku  katika jamii na na kuvuruga amani nchini.
‘’’’Tuhakikishe tunazungumzia mikoa yetu kwa Taarifa sahihi zenye ukweli na kujenga  na zilizohakikiwa na wahusika na siyo kutoa taarifa za kutunga ambazo zinaweza leta tafrani ndani ya nchi’’alisema
Kwa upande wake katibu tawala wa mkoa wa aIringa Wamoja Ayubu akisoma taarifa ya mkoa wa Iringa kwa katibu mkuu kuhusu hali ya utekelezaji wa  sekta ya habari,sanaa,utamaduni na michezo kwa mkoa wa Iringa  alisema Sekta ya Habari ina jukumu la kusimamia utekelezaji wa Serra ya Habari na Utangazaji ya mwaka 1993 na Sheria zinazohusu masuala ya Habari ususani Kuunganisha vyombo vya habari na Serikali katika kufikia taarifa, maelekezo na maagizo ya serikali kwa jamii.
“””””””””’’’’’’Sekretarieti ya Mkoa inaendelea na utekelezaji wa majukumu ya sekta ya Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo  kwa Kuratibu utekelezaji wa shughuli za Maafisa Habari katika Mamlaka za Serikali za Mitaa. Kuwezesha maandalizi na utekelezaji wa kampeni mbalimbali za kiserikali katika mkoa wa Iringa.Kusaidia katika ufafanuzi wa Sera mbalimbali za Serikali kupitia machapisho na majadiliano pamoja na wadau,Kuratibu machapisho ya makala maalumu na habari zinazohusu maendeleo ya mkoa wa Iringa kwa lengo la kutangaza huduma zitolewazo na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa.’’’alisemawamoja.
Wamoja alisema Maafisa Habari katika Mamlaka za Serikali za Mitaa wameweza kutekeleza majukumu yao ya kihabari kwa ufanisi zaidi na wananchi kunufaika na huduma hiyo,na hatimae kupelekea manufaa makubwa katika sekta ya sekta ya habari,sanaa,utamaduni na michezo kwa mkoa wa Iringa.

Alisema mkoa wa Iringa umekuwa na ongezeko  la vituo vya redio vinavyomilikiwa na sekta binafsi na taasisi hadi kufika vituo saba (7) katika Mkoa wa Iringa. Ongezeko hilo limepanua  wigo wa upatikanaji wa habari kiurahisi kwa wananchi na kuwezesha uhuru wa kuchagua aina ya chombo cha habari na aina ya habari ya kusikilizwa ,hivyo kukuza uhuru wa kupata Habari mkoani Iringa.

‘’’’’’’’’’’Kutokana na usimamizi imara wa Sera ya Habari na Utangazaji ya mwaka 1993 na sheria zinazoongoza sekta ya Habari, hali ya huduma ya upatikanaji na utoaji wa Habari imekuwa nzuri katika Mkoa wa Iringa .’’’’’’’’’’’’’’’alisema.




Nae mwenyekiti wa chama cha wandishi wa habari mkoa wa Iringa[IPC]Frank Leonard ambae pia ni mwandishi wa habari katika gazeti la serikali la Habari leo, alitoa kilio chake kwa serikali  kuiomba iwabane wamiliki wa vyombo vya habari ambao hawajawaajili wandishi  wao ili waweze kutoa mikataba.
Leonard alisema wizara husika itafute namana ya kuwabana wamiliki wa vyombo vya habari   ili waweze kutoa miakataba kwa wandishi wao kwa kufanya hivyo wandishi watapata  kutasaidia tansinia hii ya habari iweze kusonga mbele.
Asilimia kubwa ya wandisghi wa habari hawana ajira maalumu,wanajitolea  na kutegemea bahasha kutoka kwa waalikwa ,hali hii ahileti ufanisi katika kazi .Naiomba serikali  kama kuna uwezekano iwakutanishe wamiliki wa vyombo vya habari na wandishi wao ili kujadili namna ya kutoa mikataba kwa wandishi wao  ambao bado hawajaajiliwa  na hatimae wandishi waweze kupata haki stahiki  kutokana na kazi wanazozifanya’’’alisema



0 maoni:

Chapisha Maoni