Mbunge
wa Jimbo la Mtama ambaye pia ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na
Michezo Mhe. Nape Nnauye akisalimiana na Diwani wa kata ya Mtama Bw.
Hassan Omary Nyimbile (CHASEMA) mara baada ya kuwasili kwenye hospitali
ya Nyangao kumjulia hali Baba wa Diwani huyo aliyelazwa hapo. .
Mbunge
wa Jimbo la Mtama ambaye pia ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na
Michezo Mhe. Nape Nnauye akipewa maelezo juu maendeleo ya hali ya Mzee
Omary Nyimbile, baba wa Diwani wa kata ya Mtama Bw. Hassan Omary
Nyimbile (CHADEMA) aliyelazwa katika Hospitali ya Nyangao.
Mbunge
wa Jimbo la Mtama ambaye pia ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na
Michezo Mhe. Nape Nnauye akimuangalia Mzee Omary Nyimbile, baba wa
Diwani wa kata ya Mtama Bw. Hassan Omary Nyimbile aliyelazwa katika
hospitali ya Nyangao.
………………………………………………………………………………………
Mbunge
wa Jimbo la Mtama ambaye pia ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na
Michezo Mhe. Nape Nnauye amemjulia hali Mzee Omary Nyimbile, baba wa
Diwani wa kata ya Mtama Bw. Hassan Omary Nyimbile .
Mhe. Nape ambaye yupo kwenye
ziara ya utekelezaji wa ahadi zake jimboni kwake na kuonana na wananchi
alifika kwenye hospitali ya Nyangao mwishoni mwa wiki iliyopita na
kupokelewa na Diwani huyo wa kata ya Mtama kupitia Chama Cha Chadema.
Mheshimiwa Mbunge wa Mtama alimjulia hali Mzee Omary na kumtakia heri ya kupona haraka.
Kitendo cha Mhe. Mbunge kumjulia
hali baba wa Diwani wa Chadema kimewashangaza wengi ambao walidhani
viongozi hawa hawatoweza kuzungumza kutoka na hali ilivyokuwa wakati wa
uchaguzi.
0 maoni:
Chapisha Maoni