Mbunge
wa Jimbo la Kibaha mjini Silvestry Koka akikagua moja ya sehemu ya
vibanda vya biashara vilivyopo katika eneo la maili moja baada ya
kuteketea kwa moto na kuweza kuunguza maduka matano moto huo ulizuka
hivi karibu.
Mbunge
wa Jimbo la Kibaha Mjini Silvestry Koka akimkabidhi mmoja wa wahanga
waliounguliwa maduka yao eneo la maili moja kiasi cha shilingi laki tano
ikiwa ni kuwapa msaada wa kuanzia mtaji mwingine alipofanya ziara ya
siku moja ya kuwapa pole.(PICHA NA VICTOR MASANGU)
………………………………………………………………………………………………………………………………..
NA VICTOR MASANGU, KIBAHA
WIMBI la kutokea kwa majanga ya
moto bado limeonekana bado kuwa ni tatizo sugu kutokana na kuwepo kwa
uelewa mdogo kwa wananchi kuhusiana na namna ya kuweza kuzuia majanga ya
moto pindi yananapojitokeza pamoja na kutokuwa na vifaa vya kuzimia.
Hayo yamebainishwa na Afisa
uhusiano wa Jeshi la zima moto na uokoaji Mkoa wa Pwani Harryson
Mkonyi wakati akizungumza katika mkutano maalumu wa kuwafariji na
baadhi ya wahanga ambao ni wafanyabiashara waliounguliwa maduka yao na
kuteketeza mali zao zote kwa moto katika eneo la maili moja Wilayani
Kibaha.
Mkonyi amebainsiha kuwa
wamebaini kuna baaadhi ya wananchi pindi wanapokumbwa na ajali ya moto
wanajikuta wanashindwa kuuzima na kuuzuia usiendelee kusambaa katika
maeneo mengine kutokana kutokuwa na vifaa, kuwa na uelewa mdogo juu ya
uzimaji wa moto pamoja na kuchelewa kutoa taarifa katika vyombo
vinavyohusika.
“Kwa sasa kutokana na baadhi ya
wananchi kutokuwa na uelewa juu ya kupambana na majanga ya moto pindi
yanapotokea, tumeanza kutoa elimu katika sehemu mbali mbali ili kuweza
kuwafundisha jinsi ya kuzuaia moto kwani wakati mwingine wanachelewa
kutoa taarifa kutokana na kuamua kuuzima wenyewe na unaposambaa ndipo
wanatoa taarifa,”alisema Mkonyi.
Akisoma risala kwa niaba ya
wahanga hao wa moto Tatu Jamaly pamoja na mmoja wa wafanyabishara
waliokumbwa na majanga hayo ya moto Marietha Massaji wamesema kwamba kwa
sasa wamejikuta katika wakati mgumu sana kutokana na biashara ambazo
walikuwa wanazitegemea kwa ajii ya kujipatia kipato cha kila siku
imeteketea yote kwa moto huo.
“Tulikuwa na tunafanya biashara
zetu na zilikuwa zinatusaidia sana katika kujipatia kipato lakini ndio
hivyo tena tumepata majanga ya moto na mali zetu zote zimeteketea,
lakini tunamshukuru sana mbunge wetu wa jimbo la Kibaha mjini Silvesty
Koka kwa kwa moyo wake wa dhati kwa kutuchangia fedha amabazo
zitatusaidia kuanza tena biashara zetu,”alisema Wahanga hao.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa
serikali ya mtaa wa maili moja Athumani Chichi alisema kwamba kutokana
na wafanyabishara hao kupatwa na matatizo wamerudishwa nyuma kimaendeleo
na kuongeza kwamba ataendelea kushirikiana na mbunge wa jimbo la Kibaha
kwa hali na mali kutokana na kupenda maendeleo na kuwasaidai wananachi
wake pindi wanapopata matatizo.
Naye Mbunge wa jimbo la Kibaha
mjini Silvestry Koka ambaye alifanya ziara ya kuwatembelea wahanga hao
wa moto ambapo amewaasa amewachangia kiasi cha shilingi laki tano kwa
kila mfanyabiashara ambaye duka lake limeungua na moto na kuwaasa
kutokukata tamaa na badala yake mtaji mwingine huo aliowapatia
wautumie vizuri katika kukuza biashara zao na sio vinginevyo.
Koka alisema kwamba anatambua
uchungu walionao wahanga hao ambapo ameahidi kuendeea kuwasaidia na
kushirikiana nao bega kwa bega katika kuhakikisha wanatimiza malengo yao
kupitia shughuli zao za ujasiliamali wanazozifanya.
MOTO huo ambao ulizuka katika
eneo la maili moja Wilayani Kibaha Mkoa wa Pwani umeweza kuteketeza
maduka matano pamoja na mali za wafanyabiashara,wa aina mbali mbali
lakini haukuweza kuleta madhara yoyote kwa binadamu .
0 maoni:
Chapisha Maoni