Mkuu
wa Chuo cha Elimu Biashara (CBE) Prof. Emmanuel Mjema akiwaonesha
waandishi wa habari (hawapo pichani) ripoti ya Mamlaka ya Udhibiti ya
Manunuzi ya Umma (PPRA) ya Mwaka huu inayoonesha chuo hicho ni moja kati
ya Taasisi 14 zilizofanya vizuri kwa kushika nafasi ya kwanza kwa
kupata alama 95.8 katika kufuatilia sheria ya manunuzi ya umma na
kuutaka umma kupuuza taarifa za upotoshaji zinazotolewa na baadhi ya
watu kuwa wanakiuka sheria hizo.PICHA NA HASSAN SILAYO-MAELEZO.
Mkuu
wa Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) Prof. Emmanuel Mjema akiwaonesha
waandishi wa habari (hawapo pichani) ripoti ya Mdhibiti na mkaguzi mkuu
wa hesabu za serikali (CAG) inayoonesha kuwa chuo hicho kimepata ziada
ya bilioni 1.2 kati ya mwaka huu na kufanya chuo kujiendesha kwa faida
tofauti na baadhi taarifa za upotoshaji zilizotolewa na baadhi ya vyombo
vya habari.
………………………………………………………………………………………………………………………
Frank Mvungi-Maelezo
Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE)
kimewataka wananchi kupuuza taarifa za upotoshaji zilizoripotiwa na
Baadhi ya vyombo vya Habari Hapa nchini kuhusu chuo hicho.
Akizungumza na vyombo vya Habari
leo jijini Dar es salaam Mkuu wa chuo hicho Prof. Emmanuel Mjema amesema
tuhuma za kuwa chuo hicho kina ubadhirifu wa kutisha si za kweli na
zinalenga kuchafua taswira ya chuo hicho.
“Chuo kinafanyiwa ukaguzi wa
Hesabu zake na Mkaguzi na Mdhibiti wa hesabu za Serikali na kwa kipindi
cha miaka minne tumepata hati safi (Clean Audit Report) kuanzia mwaka
2010/2011 hadi 2014/2015 .” alisisitiza Prof. Mjema.
Katika ukaguzi huo ripoti hiyo
ilionyesha kuwa Taasisi hiyo imekuwa ikizingatia sheria na kanuni za
matumizi ya fedha za umma hali iliyopelekea kupata hati safi kwa kipindi
chote.
Pia Chuo hicho kilifanyiwa
ukaguzi na Mamlaka ya Udhibiti wa manunuzi Serikalini (PPRA) kwa mwaka
unaoishia 2014/2015 na Chuo hicho kupata alama 95.8 hivyo kuwa moja ya
Taasisi za Umma zinazofanya vizuri katika kuzingatia sheria na kanuni za
manunuzi ya umma.
Prof. Mjema amesema kuwa chuo
hicho kimekuwa kikijiendesha bila kupata ruzuku toka Serikalini na pia
kuzalisha mapato ya ziada zaidi ya bilioni moja kwa kwa kila mwaka wa
fedha kuanzia mwaka 2013 hadi 2015.
Kutokana na Mafanikio hayo chuo
hicho kimeweza kuanzisha Kampasi ya Mbeya ambapo chuo hicho kimenunua
eneo lenye ukubwa wa ekari 54.9 na pia maboresho katika maktaba ya chuo
yamefanyika.
Mafanikio mengine ni kujenga hema
kubwa lenye uwezo wa kuchukua wanafunzi 740 na kuboresha karakana ya
vipimo na mizani chuoni hapo.
0 maoni:
Chapisha Maoni