Bw.Tesha
Philemon Kaimu Mkurugenzi wa KItengu cha Huduma za Kibenki Mtandaoni
Benki ya UBA kushoto akibadilishana mikataba na Bw. Mike Raymond
Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Regency Innovation Solutions baada ya
kusaini mkataba wa kutoa huduma ya kadi ya malipo ya kipekee ya Visa
inayoitwa Mimosa Black Card leo kwenye hoteli ya Regency Park Mikocheni
jijini Dar es salaam.
Bw.Tesha
Philemon Kaimu Mkurugenzi wa Kitengo cha Huduma za Kibenki Mtandaoni
Benki ya UBA kushoto na Bw. Mike Raymond Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni
ya Regency Innovation Solutionswakionyesha kadi ya malipo ya kipekee ya
Visa inayoitwa Mimosa Black Card iliyozinduliwa leo baada ya kampuni
hizo kutiliana sahihi mkataba wa kufanya biashara kwa pamoja.
Bw.Tesha
Philemon Kaimu Mkurugenzi wa Kitengo cha Huduma za Kibenki Mtandaoni
Benki ya UBABw.Takizungumza katika mkutano huo uliofanyika kwenye hoteli
ya Regency Park Mikocheni jijini Dar es salaam.
………………………………………………………………………………………………………………..
Kampuni ya uvumbuzi na suluhisho
inayoitwa Regency Innovation Solutions na benki ya UBA ya Tanzania
wamesaini mkataba wa maelewano wa kutoa huduma ya kadi ya malipo ya
kipekee ya Visa katika bara zima la Afrika wakianzia nchini Tanzania.
Taarifa hii imetolewa leo katika mkutano na waandishi wa habari
uliofanyika jijini Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa kadi mpya ya
malipo itakayoitwa Mimosa Black Card, kadi ambayo itaruhusu mteja kuweka
na kutoa fedha bila ya kuhitaji akaunti ya benki.
Mkurugenzi Mkuu wa Regency
Innovation Solution Mike Raymond alisema “Tumefurahi kushirikiana na
benki ya UBA Tanzania katika uendelezaji wa uvumbuzi ambao utaanzia hapa
Tanzania. Lengo letu ni kuleta suluhisho zilizo salama na kuaminika kwa
wateja wetu. Kadi hii ya Mimosa ni ya kisasa ambayo sio tu ni salama na
inayorahisisha huduma bali ina huduma nyingine nyingi na zawadi kwa
wateja. Kupitia huduma hii tunaongeza wigo wa huduma za kifedha katika
nchii ya Tanzania haswa kwa sababu kadi hii imeunganisha na huduma za
pesa kupitia mitandao ya simu.”
Kadi hii mpya ni sawa na kadi ya
kawaida ya malipo ya kabla ila ni ya kipekee kwa sababu haiunganishwi na
akaunti ya benki hivyo kuifanya kuwa ya gharama nafuu na pia urahisi wa
kuweka na kutoa fedha. Kadi hii pia italindwa kwa neno la siri (PIN) na
teknolojia ya juu ya ulinzi. Kwa maana hiyo watumiaji wa kadi ya Mimosa
wanaweza kutoa fedha katika mashine za kutolea fedha (ATM), kufanya
malipo ya kutumia kadi katika maeneo yote yenye huduma hiyo na pia
kufanya manunuzi mtandaoni mahali popote duniani kupitia mtandao wa
Visa. Vile vile wateja wanaweza kuweka pesa katika kadi zao kupitia
tawi lolote la UBA Tanzania au mitandao ya simu M-pesa, Tigo Pesa,
Airtel Money na pia katika akaunti za kukusanya fedha katika benki za
CRDB na Exim.
“Tanzania tayari ina mfumo wa
teknolojia ya kuwa jamii isiyotumia fedha. Kupitia kadi zetu
tunawahamasisha wateja wetu kupokea mfumo huu wa kufanya malipo bila
kutumia fedha. Zaidi ya hapo wateja wetu watapata punguzo la bei katika
baishara mbalimbali sio tu Tanzania bali barani Afrika na baadaye
ulimwengu mzima watakapofanya manunuzi kupitia kadi hizo. Wateja pia
wanaweza kupata fedha za dharura hadi shillingi Milioni moja kwa riba ya
asilimia sifuri,” aliongeza Raymond.
Naye Kaimu Mkuu wa Kitengo cha
Huduma za Fedha za Kielektroniki wa UBA Tanzania, Tesha Philemon,
alisema kuwa “ Lengo letu kuu ni kubadilisha mfumo wa jinsi watu
wanavyotumia huduma za kibenki haswa kwa kujikita katika kundi la wale
ambao hawatumii huduma za benki kwa kupitia teknolojia kama hizi.
Tunaamini kuwa ushirikiano huu kati ya UBA Tanzania na Regency
Innovation Solutions utafanikisha lengo letu la kuwafikia wale
wasiotumia huduma za benki na kuwajumuisha katika huduma hizi katika
Tanzania na bara la Afrika.
Tanzania ni nchi ya kwanza katika
ushirika huu kuanza kutumia teknolojia hii. Kampuni ya Regency
Innovation Solutions tayari ina miradi kama hii katika nchi za Zambia na
Uganda na wana mpango mkubwa wa kuleta mabadiliko makubwa katika kutoa
vitambulisho kwa kutoa vitambulisho vya ushirika vya Visa kwa wanafunzi
na makampuni na katika siku za karibuni pia watazindua kadi za malipo
kabla za Visa za Dhahabu na Platinum.
Fursa
- Kuwa wakala wa usambazaji wa kadi hizi tafadhali tuma barua pepe kwa Meneja wa Akaunti kupitia : RegencyInnovation@gmail.com
- Kusajili kampuni yako kuwa katika orodha ya biashara zitakazotoa punguzo kwa wateja zaidi ya 500 wa kadi za Mimosa, tutumie barua pepe kwa Meneja wa Akaunti kupitia : RegencyInnovation@gmail.com
0 maoni:
Chapisha Maoni