Fainali
za Kombe la Shirikisho maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC)
zinatarajiwa kufanyika kesho Mei 25, 2016 kwa kuzikutanisha timu za
Young Africans na Azam FC; zote za Dar es Salaam katika mchezo
utakaofanyika Uwanja wa Taifa jijini.
Sherehe
za mchezo huo zitaanza rasmi saa 8.00 mchana kwa mchezo wa awali wa
kuburudisha kuzikutanisha timu za soka za kituo cha Televisheni cha Azam
‘Azam Tv’ na wafanyakazi wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) na
kurushwa live na kituo hicho kilichotokea watazamaji wa nchi za Afrika
Mashariki na Kati.
Viingilio
katika mchezo huo itakuwa ni Sh 25,000 kwa VIP A wakati VIP B na C ni
Sh 20,000 wakati majukwaa yenye viti vya rangi ya chungwa, mzunguko
wenye viti vya rangi ya bluu na kijani ni Sh 5,000.
TFF
inajivunia nyota wake kama Jemedari Said, Wilfred Kidao, Salum Madadi,
Alfred Lucas, Danny Msangi, Michael Ngogo na Jonas Kiwia, lakini Meneja
wa timu ya Wafanyakazi wa TFF, Eliud Mvella anasikitika kumkosa nyota
wake Mwesigwa Selestine.
Azam
Tv wanatamba na nyota wao waliopata kufanya kazi nje ya nchi katika
vyombo vya kimataifa kama vile Charles Hilary, Tido Mhando, Yahaya
Mohammed, Baruan Muhuza na Rhys aliyetajwa kwa jina moja.
Mbali
ya burudani hiyo, pia Mwakilishi wa Azam Tv, Baruan Muhuza alisema
kwamba mara baada ya mchezo huo utakaomalizika saa 9.00 alasiri,
itafuata burudani ya wasanii mbalimbali ambao pia wataburudisha wakati
wa mapumziko ya mchezo huo.
Alisema
kwamba burudani hiyo itakuwa ni ya nusu saa kabla ya kuziacha timu
kufanya maozezi ya kupasha moto viungo kabla ya mchezo huo kuanza saa
10.30 jioni na wakati wa mapumziko burudani itaendelea kabla ya kutolewa
taji ambalo timu zitakuwa zikiliwania.
Kwa
mujibu wa kanuni bingwa wa michuano hiyo atatwaa kombe, medali na fedha
Sh 50,000,000 wakati mshindi wa pili atazawadiwa tuzo na medali.
Kadhalika kutakuwa na tuzo kwa mchezaji bora, mfungaji bora na mchezaji
bora wa michuano hiyo ambayo waaandaaji wamepanga kuiboresha mwakani.
Mwamuzi
wa mchezo huo atakuwa Israel Mujuni Nkongo wa Dar es Salaam kwa mujibu
wa Kamati ya Waamuzi ya TFF huku akisaidiwa na Ferdinand Chancha wa
Mwanza upande wa kulia (line 1) na upande wa pili ni Soud Lila wa Dar es
Salaam (line 2) na mwamuzi wa akiba mezani ni Frank Komba wa Dar es
Salaam pia. Kamishna wa mchezo huo anatakuwa Juma Mgunda wa Tanga.
Kwa
mujibu wa kanuni za Ligi Kuu msimu 2015/16, mabingwa wa Ligi Kuu ya
Vodacom Tanzania Bara msimu 2015/16 wataiwakilisha nchi katika michuano
ya Ligi ya Mabingwa Afrika msimu wa 2016/17. Nafasi hiyo imechukuliwa na
Young Africans.
Kadhalika
Azam ina tiketi tayari ya kushiriki Kombe la Shirikisho Barani Afrika
kwa kufika fainali za ASFC ingawa kanuni zinataka bingwa ambako kwa
upande wa Yanga wana tiketi ya michuano ya juu zaidi ya shirikisho.
Mvuto wa mchezo wa Jumatano ni ushindani wa soka na zawadi kwa bingwa.
Fainali
za Kombe la Shirikisho zinakuja baada ya mchuano ulioshindanisha timu
64 za Ligi Kuu Tanzania Bara – VPL (16); Ligi Daraja la Kwanza -FDL
(24), Ligi Daraja la Pili – SDL (24).
0 maoni:
Chapisha Maoni