Jumanne, 17 Mei 2016

MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA AFUNGUA MKUTANO WA UHAWILISHAJI FEDHA KWA KAYA MASIKINI AFRIKA NA KUKABIDHI HUNDI ZA MADAWATI

sm1Washiriki wa Mkutano wa kwanza wa Mifuko ya Maendeleo ya Jamii TASAF kuhusu mpango wa Uhawilishaji wa Fedha na kunusuru kaya masikini kwa Nchi Jumuiya ya Afrika wakimsikiliza Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, alipokua akifungua mkutano leo Mei 16, 2016 katika Hoteli ya Ngurudoto Mjini Arusha.                           
sm2Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na Wajumbe wa Mkutano wa kwanza wa Mifuko ya Maendeleo ya Jamii TASAF kuhusu mpango wa Uhawilishaji wa Fedha na kunusuru kaya Masikini kwa Nchi Jumuiya za Afrika uliofunguliwa leo Mei 16, 2016 katika Hoteli ya Ngurudoto Mjini Arusha.
sm01Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejiment ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Angela Kairuki kabla ya kufungua Mkutano wa kwanza wa Mifuko ya Maendeleo ya Jamii TASAF kuhusu mpango wa Uhawilishaji wa Fedha na kunusuru kaya masikini kwa Nchi Jumuiya ya Afrika wakimsikiliza Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, alipokua akifungua mkutano leo Mei 16, 2016 katika Hoteli ya Ngurudoto Mjini Arusha.
sm4Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza na Mkurugenzi wa Benki ya Dunia anaeshuhulikia Nchi za Tanzania, Burundi, Malawi na Somalia Bibi. Bella Bird walipokutana katika ukumbi wa Mikutano wa Ngurudoto Mjini Arusha leo Mei 16, 2016, ambapo Makamu wa Rais alifungua mkutano wa kwanza wa TASAF kuhusu Uhawilishaji wa Fedha na kunusuru kaya masikini kwa Nchi Jumuiya ya Afrika.
sm5Makamu wa Rais wa Jamhuri uya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akikabidhi Hundi kwa Mkuu wa Mkoa wa Songwe Mhe. Chiku Galawa kwa ajili ya kukabiliana na uhaba wa Madawati. Jumla ya  Madawati Elfu 16.5 yenye thamani ya Tshs. 1 Bilioni moja zilikabidhiwa kwa Wakuu wa Mikoa inayozunguka Mbuga ya Hifadhi ya Taifa kwa ajili yakukabiliana na tatizo la Madawati kwenye Shule zote zilizomo katika Wilaya za Mkoa hiyo. Makabidhiano hayo yamefanyika leo Mei 16,2016 katika ukumbi wa Ngurudoto mjini Arusha.katikati waziri wa Maliasili Utalii Profesa Jumanne Magembe.       sm6Makamu wa Rais wa Jamhuri uya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akikabidhi Hundi kwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. John Mongela  kwa ajili ya kukabiliana na uhaba wa Madawati. Jumla ya Madawati Elfu 16.5 yenye thamani ya Tshs. 1 Bilioni moja zilikabidhiwa kwa Wakuu wa Mikoa inayozunguka Mbuga ya Hifadhi ya Taifa kwa ajili yakukabiliana na tatizo la Madawati kwenye Shule zote zilizomo katika Wilaya za Mkoa hiyo. Makabidhiano hayo yamefanyika leo Mei 16,2016 katika ukumbi wa Ngurudoto mjini Arusha. Katikati waziri wa Maliasili Utalii Profesa Jumanne Magembe (Picha na OMR)

0 maoni:

Chapisha Maoni