Serikali
imesema kuwa mtu yeyote atakayekamatwa kwa kosa la husisha au
kushawishi mtoto kujiingiza katika matumizi au biashara ya dawa za
kulevya atahukumiwa kifungo cha miaka isiyopungua 30.
Hayo
yamesema na Mkuu wa Kitengo cha Elimu, Habari na Takwimu wa Tume ya
kuratibu na kudhibiti wa Dawa za Kulevya, Amani Msami kupitia Taarifa ya
tume hiyo kwa vyombo vya habari.
Msami
alisema adhabu hiyo ni kwa mujibu wa Sheria ya kudhibiti na kupambana
na Dawa za Kulevya Na.5 ya mwaka 2015 tofauti na Sheria ya Kuzuian
Biashara Haramu ya Dawa za Kulevya Na. 9 ya mwaka 1995 iliyokuwa na
mapungufu.
Alisema
mbali na adhabu hiyo, sheria hiyo mpya imeweka adhabu ya kifungo cha
maisha na faini ya shilingi Milioni 200 kwa kumiliki mitambo ya
kutengeneza dawa za kulevya.
Msami
aliongeza kuwa Sheria hiyo pia imeweka adhabu kali ya kifungo cha
maisha pamoja na faini isiyopungua Shilingi Bilioni moja kwa watu
wanaofadhili biashara ya Dawa za Kulevya.
“Aidha,
sheria hii imeweka adhabu kali ya kifungo cha maisha pamoja na faini
isiyopungua Shilingi Bilioni moja kwa watu wanaofadhili biashara ya Dawa
za Kulevya ambao mara nyingi ni watu wenye uwezo,” alisema Msami.
Mkuu
huyo wa Kitengo, alisema Serikali kupitia vyombo vya Dola iliwabaini,
kuwakamata na kuwachukulia hatua za kisheria baadhi ya wafanyabiashara
wadogo na wakubwa wa dawa za kulevya.
Aliwataja
baadhi ya watuhumiwa wakubwa wa dawa hizo waliokamatwa na kuchukuliwa
hatua kuwa ni Ali Khatibu haji (maarufu kwa jina la Shkuba, Mohammed
Mwarami (maarufu kwa jina la Chonji na Mwanaidi Mfundo (maarufu kwa jina
la Mama Leila).
Msami
alisisitiza wito wa Serikali kwa wananchi kutoa ushirikiano wa dhati
kwa ajili ya kutoa taarifa kuhusu watu wanaojihusisha na biashara ya
dawa ya kulevya ili waweze kuchukuliwa hatua za kisheria.
Anitha Jonas – MAELEZO
0 maoni:
Chapisha Maoni