UPUNGUFU wa wafanyakazi
kwenye wodi ya wazazi katika Hospitali ya Wete unaweza kuleta athari
kwa mama wajawazito na wazazi kutokana na kitendo cha kutumia kitanda
kimoja watu wawili .
Hayo yalibanika baada ya Mkuu
wa Mkoa wa Kaskazini Pemba Omar Khamis Othman kufanya ziara ya
kushitukiza katika Hospitali , na kuelezea kusikitishwa na kitendo cha
mama wazazi kuchangia kitanda kwa wakati mmoja .
Akizungumzia changamoto hiyo Dk
Mbwana Shoka Salim alisema kuwa pamoja na uwepo wa jengo jengine ambalo
limejengwa kwa ajili ya wazazi , lakini limeshindwa kutumika kutokana
na upungufu wa wafanyakazi .
Awali Mkuu wa Mkoa alitaka
ufafanuzi wa mama wazazi kuchangia kitanda kimoja wakiwa wawili , wakati
jengo lina nafasi kubwa kutosheleza mahitaji ya mama wanakwenda
kujifungua katika hospitali hiyo .
Dk Mbwana alisema , mama mzazi
na mtoto anatakiwa kuwa chini ya uangalizi wakati wote , na kwamba
kitendo cha kuhamia jengo jengine itakuwa ni ufumbufu katika kutoa
hudumia kwa daktari atakaye kuwa zamu .
“Jengo lipo lakini tatizo ni
wafanyakazi , unajua mama mzazi na mtoto anatakiwa kuwa chini ya
uangalizi wakati wote , hivyo kuwahamishia jengo jengine itakuwa ni
usumbufu katika utojai wa huduma ”alifahamisha.
Naye daktari Bikombo Abdalla
alikiri kwamba kitendo cha kuchangia kitanda kimoja wazazi wawili
kunahatarisha maisha ya mama na mtoto kwani baadhi yao wamejifungua kwa
njia ya upasuaji .
“Ni kweli hali hii inahatarisha
maisha ya mama na mtoto kwani baadhi yao wamejifungua kwa njia ya
upasuaji , tunaiomba Serikali ya Mkoa kusaidia kupatikana wataalamu wa
kutosha ili tuweze kutoa huduma vyema ”alieleza.
Katika nasaha zake , Mkuu wa
Mkoa mbali na kusikitishwa na kitendo cha wazazi kuchangia kitanda watu
wawili , pia aliwataka madaktari kutumia lugha nzuri wakati wanapotoa
huduma kwa wateja wao .
Alisema , baadhi ya madaktari
wanapohudumia wagonjwa hutumia lugha chafu jambo ambalo husababisha
lawama kwa Serikali kutokana na kosa la mtu mmoja .
“Tumieni lugha nzuri wakati
mnapohudumia wagonjwa , ili kupunguza lawama kutoka kwa wagonjwa pamoja
na wananchi wanaoleta wagonjwa wao hospitalini hapa ”alisema Mkuu wa
Mkoa .
Hivyo ameahidi kumchukulia hatua za kisheria daktari ambaye atabainika kutumia lugha mbaya na vitisho kwa wagonjwa .
0 maoni:
Chapisha Maoni