Mwandishi maalum-Geneva
Tanzania imekua miongoni mwa nchi chache katika bara la Afrika kufanikiwa kufikia lengo la nne la maendeleo ya millennia la kupunguza vifo vya watoto chini ya miaka mitano.
Tanzania imekua miongoni mwa nchi chache katika bara la Afrika kufanikiwa kufikia lengo la nne la maendeleo ya millennia la kupunguza vifo vya watoto chini ya miaka mitano.
Hayo yamesemwa na waziri wa
afya,maendeleo ya jamii ,.jinsia,wazee na watoto Ummy mwalimu wakati
akihutubia mkutano wa 69 wa afya duniani unaofanyika nchini
Geneva,Uswisi.
Ummy alisema licha ya kukabiliwa
na changamoto mbalimbali Tanzania imepiga hatua katika sekta ya afya
kwa kupunguza vifo hivyo hadi kufikia vifo 54 kati ya vizazi hai 1,000
kutoka vifo 112 kati ya vizazi hai 1,000
Aidha, mkutano huo ambao ni wa
ngazi ya juu katika sekta ya afya duniani, Tanzania imetambuliwa na
kutangazwa kuwa miongoni mwa nchi zilizotokomezwa ugonjwa wa polio kwa
kufanikiwa katika utoaji wa huduma za chanjo nchini kwa watoto.
“Ninaeleza kwa masikitiko kuhusu
tatizo la mlipuko wa ugonjwa wa kipindupindu uliopo nchini Tanzania
ambapo hadi kufikia tarehe 22 Mei, 2016 idadi ya wagonjwa ilifikia
21,581,kati yao watu 338 wamepoteza maisha,naahidi Serikali kupitia
wizara ya afya itaimarisha na kuzingatia kanuni za afya ya mazingira
katika kukabiliana na ugonjwa huu”alisema
Kwa upande wa kutokomeza malaria
waziri Ummy alisema Tanzania imeweza kupunguza maambukizi ya ugonjwa
huu kutoka asilimia 18 hadi 9.5 kwa Tanzania bara na kwa upande wa
Zanzibar imefanikiwa kupunguza idadi ya wagonjwa hadi kufikia asilimia
0.6 .
Katika kuboresha huduma za afya
nchini alisema Serikali ya Tanzania imejipanga na kuhakikisha itaboresha
huduma za afya ziweze kumfikia kila mtanzania popote alipo, “ili
kuweza kufikia malengo haya ni wakati muhimu sasa kuwekeza zaidi katika
sekta hii kwa kuongeza uwekezaji katika raslimali fedha,watu pamoja na
kuboresha miundombinu ikiwemo utoaji wa huduma za afya nchini”.
Waziri Ummy alisema katika
kufikia mafanikio ,wizara ya afya inatarajia kuwasilisha muswada wa
sheria katika bunge la mwezi wa Septemba,2016 wa kila mtanzania kuwa na
bima ya afya kitu ambacho kitakuwa ni mkombozi mkubwa kwa mwananchi
katika kupata huduma za matibabu wakati wowote anapokuwa na fedha au
kutokuwa na fedha kwa kuwa maradhi hayachagui wakati.
Mkutano mkuu wa mwaka wa Afya
Duniani hufanyika nchini Geneva –Uswis kila mwaka mwezi mei ambao
huwakutanisha mawaziri wa afya kutoka nchi wanachama wa Shirika la
afya Duniani {WHO} na kuhudhuriwa na wadau,mashirika na taasisi
zinazoshiriki katika kutoa huduma za afya Duniani.Tanzania inawakilishwa
na waziri wa afya Tanzania bara Mhe.Ummy mwalimu na Waziri wa Afya
Zanzibar Mhe. Mahmoud Kombo.
0 maoni:
Chapisha Maoni