Polisi
nchini Bolivia wamepambana na waandamaji walemavu ambao walikuwa
wakijaribu kwenda ikulu kudai nyongeza za mafao.Serikali ya Bolivia
imesema polisi wamepambana na waandamaji hao kwa kutumia maji ya kuwasha
mwilini walipovamiwa na kundi la waandamanaji ambao walijaribu kuvuka
mpaka uliowekwa na kujaribu kuvamia polisi kwa kutumia visu.
Waandamanaji
hao wameweka kambi katika uwanja wa La Paz kwa muda wa mwezi mmoja
sasa.Waandamanaji hawa wamekasirika baada ya vurugu kutokea.
"haya
ndio maisha tunayoishi. Tulichoomba ni kupewa hadhi kwa watu wenye
ulemavu na hiki ndio rais wa Bolivia anachofanya. Hivi ndivyo
anavyotaka, polisi kutupiga na kutudhalilisha."
Raia hao wanaoishi na ulemavu wanadai ongezeko la mafao yao ili kufikia angalau dola kumi na nne kwa mwezi.
|
0 maoni:
Chapisha Maoni