Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo Majid Hemed Mwanga,kulia mwenye miwani. akimkabidhi mwalimu mkuu wa shule ya msingi Majengo madawati.
Na Athumani Shomari, Bagamoyo.
Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo Majid HEmedi
Mwanga amekabidhi madawati 50 kwa shule mbili za msingi ikiwa ni mkakati
wa mkuu wa mkoa wa Pwani Mhandisi Everisti Ndikilo wa kuondoa uhaba wa
madawati unaozikabili shule za mkoa wa Pwani.
Madawati hayo 50 yenye thamani ya
shilingi milioni nne yamekabidhiwa kwa shule za msingi Majengo na
Mbaruku zote za Bagamoyo mjini.
Majidi amewashukuru wadau wa maendeleo
ya elimu wilayani Bagamoyo ikiwemo kampuni ya Kirai Pateli ambayo ndiyo
imetoa madawati hayo 50 ili kuondoa tatizo hilo kwa shule za serikali
huku Shubashi Pateli amtoa ahadi ya kutengeneza madawati yote
yanayohitajika kwa shule za Bagamoyo ambayo ni 1,353.
Ili kwenda sambamba na agizo la mkuu wa
mkoa wa Pwani ambae amesema mpaka kufikia tarehe 30 may shule zote za
mkoa wa Pwani ziondokane na uhaba wa madawati.
Aidha, amewataka wadau mbalimbali wa
maendeleo ya elimu wilayani Bagamoyo kuendelea kuchangia mahitaji
mbalimbali ya elimu katika wilaya ya Bagamoyo na kuongeza kuwa mara
baada ya kukamilisha madawati yanayhitajika kwa shule zote wilaya
imepanga kuanza kazi ya umaliziaji wa maabara za shule hivyo michango
inahitajika kutoka kwa wadau mbalimbali ili kufikia malengo.
Kati ya madawati hayo 50 ishirini na
manane yamekabidhiwa kwa shule ya msingi Majengo huku Ishirini na mawili
kukabidhiwa kwa shule ya msingi Mbaruku na kumaliza tatizo la madawati
kwa shule hiyo ya Mbaruku.
Awali akiongea mbele ya mkuu wa wilaya
mkuu wa shule ya msingi Majengo Andulile Lukama amesema shule ya Majengo
ina madawati 250 na ina upungufu wa madawati 109 na kwamba inakabiliwa
pia na upungufu wa vyumba vya kusomea hali inayopelekea wanafunzi
kuingia kwa zamu ambapo darasa la nne na la sita wanalazimika kutoka saa
saba ili kuwapisha darasa la tano na la tatu.
Aidha, mwalimu mkuu huyo wa shule ya
msingi Majengo Andulile Lukama na mwalimu mkuu wa shule ya msingi Anna
Kisonso wamemshukuru mkuu huyo wa wilaya kwa juhudi ya kutafuta wahisani
ili kusaidia kuondoa changamoto zinazozikabili shule za serikali
wilayani hapa.
Wakati huohuo Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo
Majid Hemed Mwanga, amewataka walimu wakuu wa shule zote za Bagamoyo
kuacha tabia ya kutumia madawati ya shule kwa shughuli za mikutano ya
hadahara.
Majid amesema kuwa madawati ni kwaajili
ya wanafunzi kusomea hivyo ni marufuku kuytatumia kwaajili mikutano
ambayo haihusiani na shule.
Amesema kitendo cha kutoa madawati nje
kwaajili ya mikuatano mbalimbali kinachangia uharibifu wa madawati hayo
na baadae kupelekea usumbufu kwa wanafunzi.
0 maoni:
Chapisha Maoni