Alhamisi, 26 Mei 2016

UPATIKANAJI WA NISHATI YA UHAKIKA NA YA BEI NAFUU NI UAMUZI NA UTEKELEZAJI WA KUDUMU




BINADAMU NA UMEME
Historia inatufundisha kwamba Wayunani (Ancient Greeks) waligundua
umeme uliotuama (static electricity) Mwaka 600 BC.
Mwaka 1752
Benjamin Franklin (UK) alifanya majaribio ya kisayansi na kuonyesha
kwamba radi (lightning) na spaki za umeme (tiny electric sparks) ni kitu
kimoja.
Mwaka 1800 Alessandro Volta (Italy) alitengeneza betri ya
kwanza kwa kutumia kemikali (an early electric battery), na Mwaka 1831
Michael Faraday (UK) alitengeneza dynamo ya kwanza (electric dynamo
– a crude power generator).
Mwaka 1879 Thomas Edison (USA) aliweza
kutengeneza balbu kwenye maabara yake (produced a reliable, longlasting electric light-bulb in his laboratory).
Jiji la New York (1880-
wakazi: milioni 1.21) lilipata taa za barabarani tarehe 4 Septemba 1882
(Pearl Street Station - electric power plant began operating) kutoka kwa
Kampuni ya Thomas Edison (USA) na Joseph Swan (UK) – hawa ndio
waliogundua, “incandescent filament light bulb” Mwaka 1878.
AINA ZA NISHATI DUNIANI (TYPES OF ENERGY RESOURCES)
Zipo aina 2 za nishati: (i) Nishati Jadidifu (Renewable Energies) na (ii)
Nishati Isiyo Jadidifu (Non-Renewable Energies).
(i) Nishati Jadidifu - Renewable Energies: (a) maporomoko ya
maji ya mto au bwawa (hydropower), (b) jua (solar), (c)
upepo (wind), (d) jotoardhi (geothermal), (e) Mabaki ya
mimea (Bio-Energies - biomass (tungamotaka) na biogas), (f)
Mawimbi ya Bahari (Waves Energy), (g) Bavua Kubwa (maji
kujaa) ya Bahari (Tides Energy), na (h) Gesi ya Hydrojeni
(Hydrogen Energy).
Tanzania tunayo bahati ya kuwa na vyanzo vyote vya Nishati Jadidifu
isipokuwa ya aina ya “Hydrogen.” Ukame wa mara kwa mara umefanya,
baadhi ya wataalam waiondoe “hydropower” kutoka kwenye kundi hili
la Nishati Jadidifu. Tanzania imeanza kwa kasi kubwa kuviendeleza
vyanzo hivi vya Nishati Jadidifu kwa ajili ya kuzalisha umeme mwingi
zaidi.
(ii) Nishati Isiyokuwa Jadidifu, Non-Rewable Energies: (a) Makaa
ya Mawe (Coal), (b) Gesi Asilia (Natural Gas), (c) Petroleum
na (d) Nyuklia (Uranium: Nuclear Energy).
Mtaalamu pekee wa makaa ya mawe (coal) nchini, Dkt Pascal Semkiwa,
anasema kwamba tunayo makaa ya mawe ya takribani tani bilioni 10 –
utafiti unaendelea. Tunayo Gesi Asilia yenye jumla ya futi za ujazo
trilioni 56 (56 tcf) - utafutaji wa Gesi Asilia na Mafuta unaendelea na
huenda tutapata gesi nyingi sana hapo baadae.
Mashapo (deposits) ya urani nchini mwetu (Mkuju: 99.3 million pounds na Manyoni: 29 million pounds) yanakadiriwa kuwa na jumla ya kilo milioni 58.3 (128.3 million pounds = 58.3 million kg of uranium).
Tanzania imebahatika kuwa na mishapo (deposits) makubwa ya Nishati
Isiyokuwa Jadidifu ambayo yataendelea kuwa chanzo kikuu cha umeme
unaohitajika kwa ustawi wa Taifa letu.
UMEME NI UCHUMI: UHUSIANO WA UMEME NA PATO LA TAIFA
Ripoti ya IMF ya Aprili 2015 imeonyesha nchi 10 bora kiuchumi (kigezo:
Pato la Taifa, GDP) Duniani na zimeorodheshwa hapo chini.
Wingi wa umeme unaozalishwa na nchi hizo 10 umewasilishwa hapo chini. Wastani wa utumiaji wa umeme kwa mtu mmoja mmoja nao umeonyeshwa hapochini.
NB: kWh per person - wastani wa idadi za UNITI za umeme kwa mtu
mmoja mmoja kwa mwaka.
Gigawatt, (GW) 1 = 1,000 Megawatt (MW).
1. USA GDP: US$ Trillion 18.13 Installed Capacity: GW 1,064 (2012)
(2012: kWh/person: Uniti 11,919.8)
2. China US$ Trillion 11.21 GW 1,190 (21.7% ya umeme wa Dunia nzima)
(2012: kWh/person: 3,493.79)
3. Japan US$Tr 4.21 GW 289 (2012: kWh/person: 6,749.73)
4. Germany 3.41 GW 170 (2012: kWh/person: 6,696.93)
5. UK 2.85 GW 96 (2012: kWh/person: 5,467.34
6. France 2.47 GW 132 (2012: kWh/person: 7,022.63
7. India US$Tr 2.31 GW 241 (4.4% ya umeme wa Dunia nzima)
(2012: kWh/person: 498.39
8. Brazil 1.90 GW 123 (2.2% ya umeme wa Dunia nzima)
(2012: kWh/person: 2,286.26)
9. Italy 1.84 GW 123 (2012: kWh/person: 5,058.66)
10. Canada US$Tr 1.62 GW 141 (2012: kWh/person: 16,020.37)
UMEME WA TANZANIA
Tanzania inayo mitambo yenye uwezo wa kuzalisha umeme (installed
capacity) wa jumla ya MW 1,308 (27 Aprili 2015). Kwa kuwa hali yetu ya
uchumi na maendeleo wakati tunapata Uhuru (Mwaka 1961) ilikuwa
haitofautiani sana na China, Brazil na India, tunapaswa kujilinganisha na
nchi hizi ili tujipange ipasavyo kukuza uchumi, kutoa huduma kwa
wananchi na hatimae kutokomeza umaskini kama wao walivyofanya na
wanaendelea kufanya (China, Brazil and India) na kutuacha nyuma
kiuchumi – siri kubwa ya mafanikio ya maendeleo ni kujifunza kutoka
kwa aliyekuzidi au kutangulia badala ya kujifunza au kujilinganisha na
ambae unamzidi au mnalingana hali kimaendeleo au kiuchumi.
Pato kwa mtu mmoja (GDP/Capita) Umeme/kwa mtu mmoja (Power/ Capita)
China US$ 7,589 MW 1,190,000 3,493.79 kWh/person
Brazil US$ 11,604 MW 123,000 2,286.26 kWh/person
India US$ 1,626 MW 241,000 498.39 kWh/person
Tanzania US$ 1,005 MW 1,308 136.00 kWh/person
UMEME WA KUKUZA UCHUMI KWA KASI NA KUTOKOMEZA UMASKINI
Takwimu za hapo juu (China, Brazil, India na Tanzania) zinatufundisha
kwamba tunahitaji (Tanzania) umeme mwingi, wa uhakika, unaopatikana
kwa urahisi na kwa bei nafuu ili kukuza uchumi wetu kwa kasi kubwa
(zaidi ya 10%), kupatikana kwa ajira viwandani na kwenye sehemu
nyingine za uzalishaji bidhaa za biashara (k.m. kilimo, ufugaji na uvuvi),
na kutoa huduma mbalimbali kwa wananchi. Ukuaji wa uchumi huo
uanzie kwa mtu mmoja mmoja hadi ustawi wa Taifa zima.
Tumeamua (Tanzania) kuwa nchi ya kipato cha kati ifikapo Mwaka 2025.
Ikiwa tutakuwa nchi ya kipato cha kati, hali ya umeme ifikapo Mwaka
2025 inapaswa kuwa hivi:
(i) Zaidi ya Watanzania asilimia 75 (>75%) wawe na fursa ya
kutumia umeme majumbani, kwenye kilimo, ufugaji, uvuvi,
viwandani, na kwenye elimu, matibabu (afya), vyanzo vya
maji, biashara, mawasiliano, n.k.
(ii) Uchumi wa Kati wa Tanzania ifikapo Mwaka 2025, utahitaji
upatikanaji wa umeme (installed capacity) wa zaidi ya MW
10,000-15,000.
NISHATI MCHANYIKO (ENERGY MIX OR ENERGY MATRIX)
UNAOTUMIWA DUNIANI KOTE
Michoro miwili ya duara uwezo wa kuzalisha jumla ya
umeme wake mwingi kutoka kwenye makaa ya mawe (coal)
Mwaka 2012 asilimia 66 (66%) umeme wake wote utazalishwa kutoka kwenye makaa Tanzania tunayo mashapo ya makaa ya mawe (coal deposit tani bilioni 10, hivyo, Tanzania Ijayo lazima ikutoka kwenye makaa Mwaka 2025.
NI UBUNIFU
ya hapo chini inaonyesha kwamba MW 1,190,000 (2014)), itaendelea kuzalisha ke na Mwaka 2040 asilimia 52 (52%) ya tazalishwa , izalishe umeme mwingi ya mawe (coal) ili kufikia MW 10,000 China yenye
endelea coal), yaani ya mawe. deposits) zaidi ya 10,000-15,000
Brazil (jumla: MW 123,000) ni kati ya nchi chache sana Duniani zenye
nishati safi. Asilimia 80 ya umeme unaozalishwa Brazil unatokana na
Nishati Jadidifu (over 80% of the electricity generation installed capacity
in the country comes from renewable sources).
Brazil inazalisha umeme wake mwingi (angalia mchoro wa hapo juu)
kutoka kwenye maporomoko ya maji (hydropower), mafuta (petroleum:
wanayo mafuta na gesi asilia nchini mwao) na mabaki ya miwa
(bagasse) na mimea mingine (leftover fibers, stalks and leaves).
Tanzania Ijayo itaendelea kuzalisha umeme wa maji, na kuweka mkazo
wa kupata umeme wa mabaki ya miwa (bagasse) wa bei nafuu. Viwanda
vya kisasa vya sukari vinapaswa kuzalisha bidhaa zaidi ya 3: (i) sukari,
(ii) bioethanol (ethyl alcohol) – inatumika kuendesha magari, n.k. –
Brazil inaongoza Duniani, na (iii) umeme wa mabaki ya miwa (bagasse).
Umeme wa aina hii (bio-energies: mabaki ya mimea) utachangia
uzalishaji wa MW 10,000-15,000 ifikapo 2015.
Umeme mwingi wa India (jumla: MW 241,000), na kama ilivyo kwa
China, unazalishwa kutoka kwenye makaa ya mawe (55%), angalia
mchoro huo hapo juu.
TANZANIA IJAYO: itazalisha umeme kwa kutumia vyanzo vyake vyote
vilivyoainishwa hapo juu (Energy Mix or Energy Matrix): Gesi Asilia
(natural gas), Makaa ya Mawe (coal), Maporomoko ya maji
(hydropower), Jotoardhi (geothermal), Umemejua (solar), Upepo
(wind), Mawimbi ya Bahari (Waves & Tides) na Bio-Energies (biomass –
mabaki ya miwa, n.k. & biogas).
Kwa kutumia sayansi, teknolojia na ubunifu, na vyanzo vyetu vyote vya
nishati, upatikanaji wa umeme usiopungua MW 10,000 - 15,000 ifikapo
Mwaka 2025 ni jambo la LAZIMA.
Watanzania milioni 49.3 (2015), milioni 60.4 (2025) na milioni 82.7 (2050)
watahitaji umeme mwingi kwa huduma za kijamii na kukuza uchumi wao.
UMEME NI AJIRA, UMEME NI HUDUMA BORA KWA JAMII, UMEME NI
UCHUMI, UMEME HUONDOA UMASKINI

0 maoni:

Chapisha Maoni