SERIKALI imeitaka
wakala wa usajili,Ufilisi na Udhamini, RITA, kuhakikisha inatoa elimu ya
kutosha kwa wananchi kuelewa umuhimu wa kuandika wosia na mirathi ,ili
kuondoa migogoro kwa familia wakati wa kugawa mirathi ya marehemu.
Rai hiyo imetolewa jana
na mkuu wa wilaya ya Arusha, Fadhili Nkurlu, alipokuwa akifungua
kampeni ya siku NNe ya kisheria inayotolewa bure na RITA, kuhusu
kuandika mirathi na wosia na kuwaelekeza eneo salama la kuhifadhi wosia
ukisha andikwa na mhusika ili kuondoa migogoro mingi kwa familia pindi
mhusika anapofariki dunia.
Mkuu huyo wa wilaya,
alisema,wananchi wengi hawana elimu juu ya wosia na mirathi hivyo RITA,
ambayo ni wakala wa serikali ina jukumu kubwa la kuhakikisha elimu
inawafikia wengi na hivyo kuwezesha wajane na watoto ambao ndio
waathirika kupata mirathi .
Alisema wosia unasaidia
kutatua migogoro ambayo ingelijitokeza wakati wa kugawa mirathi ya
marehemu na mtu kuandika wosia sio uchuro bali ni kuweka utaratibu wa
mali za muhusika zitakavyogawiwa pindi akisha fariki dunia.
Aliikumbusha jamii kuwa
msimamizi wa mirathi sio mrithi wa mali ya marehemu bali jukumuake ni
kukusanya mali yote na madeni yote ya marehemu na kusimamia ugawaji na
ulipaji wake na kamwe msimamizi yeyote asijihusishe na urithi .
Jamii nyingi zimekuwa
zikiingia kwenye migogoro ya kugawana mirathi kutokana na kutokuwa na
elimu ya kutosha ya kuandika wosia kabla ya kifo na matokeo yake
wanaoathirika ni wajane na watoto ambao hukosa haki yao .
Awali mratibu wa
kampeni hiyo,msajili na wosia kutoka makao makuu ya RITA, Augostino
Mbuya, alisema migogoro mingi imekuwa ikijitokeza kwenye familia wakati
wa kugawa mirathi kutokana na kutokuwepo kwa wosia ambao ni mwongozo wa
jinsi ya kuigawa mali ya marehemu kwa wahusika na matokeo yake watoto na
wajane hukosa haki yao ya kurithi.
Alisema kutokana na
hali hiyo RITA, ipo tayari kutoa elimu kwa umma kuhusu huduma hiyo ya
kuandika wosia kutokana na wananchi wengi kutokuwa na elimu na kufahamu
wapi watapata huduma hiyo ya kuandika wosia na ugawaji wa mirathi za
marehemu
Mbuya,alisema mkakati
uliopo ni kusogeza huduma ya kuandika wosia na mirathi ngazi za mikoa na
wilaya pamoja na kuhakikisha wanakuwepo wanasheria wa kutosha lengo ni
kuiwezesha jamii kuondokana na migogoro ambayo inaweza kuepukwa wakati
wa kugawa mali za marehemu.
Alisema tangia
kuanzishwa kwa huduma hiyo ya Rita, imeweza kusajili wosia zaidi ya 300
na 30 kati yake zimeshachukuliwakwa utekelezaji .
Akisoma taarifa ya kazi
za Rita, msajili wa mirathi na wosia, kutoka makao makuu ya Rita,
Joseph Mwakatobe amesema mahakama kuu imeiteua RITA, kusimamia utatuzi
wa migogoro ya urithi na uandishi wa wosia lngo ni kuondoa migogoro
inayojitokeza pindi mtu anaofariki dunia.
Alisema Rita,
itaendesha kampeni hiyo ya kuhamasisha wananchi kuhusu kuandika mirathi
na wosia katika mkoa wote wa Arusha,ili kuwezesha wajane na watoto
wanapata haki yao ya kurithi mali za marehemu .
Aliongeza kuwa kuandka
wosia ni swala lahiari ya mtu,na Rita, imekuwa ikikumbana na changamoto
mbaimbali zkiwemo za kutokuwepo na wosia wakati wa mirathi .
Aliongeza kuwa mirathi
inatolewa kulingana na sheria za dini ya kiislamu, mila na sheria ya
India ya mwaka 1865 ambayo inahusisha makundi yote ambayo hayapo kwenye
makundi ya kidini na mila.
0 maoni:
Chapisha Maoni