Jumatatu, 16 Mei 2016

Mheshimiwa January Makamba akutana na wadau wa misitu

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
WADAU wa ardhi, mazingira na mambo ya misitu wanaojulikana kama Maisha Shamba
Group wameweka adhma ya kupanda miti milioni 50,000,000 ifikapo mwaka
2020, ikiwa ni mipango yao ya kutunza mazingira na kujikwamua kiuchumi
kwa kupitia sekta ya misitu nchini.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, January Makamba, akizungumza jambo katika mkutano wa wanachama wa Maisha Shamba Group wanaojihusisha na mambo ya misitu na mazingira mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.

Hayo yamesemwa na kiongozi mkuu wa group hilo, Asifiwe Malila, alipokuwa
akizungumza na wanachama wake katika mkutano wao wa mwaka, huku mgeni
rasmi akiwa ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na
Mazingira, January Makamba, mwishoni mwa wiki, katika Ukumbi wa Shule ya
Sheria Tanzania, jijini Dar es Salaam.

Mdau wa mambo ya ardhi na misitu, Ally Abdallah, akisikiliza kwa makini hutuba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, January Makamba, hayupo pichani katika mkutano wa wadau wa misitu wanaojulikana kama Maisha Shamba Group.
Naye Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, January Makamba, aliwapongeza
wadau hao wa mambo ya misitu, akiwataka waendelee kubuni mambo
yanayoweza kuwakwamua na kuisaidia nchi katika kutunza mazingira kwa
kupitia sekta ya misitu.


0 maoni:

Chapisha Maoni