Polisi
nchini Kenya inaendelea na msako wa kuutia mbaroni mtandao wa kundi la
wapiganaji la ISIS ambalo linataka kukita mizizi yake nchini Kenya kwa
lengo la kufanya mashambulizi ya kigaidi dhidi ya wananchi wasio kuwa na
hatia. Hayo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na inspekta mkuu wa
polisi .
Kauli
hiyo imetolewa baada ya polisi nchini Kenya kuwatia mbaroni watu wawili
wanaoshukiwa kuwa ni wafuasi wa kundi la wapiganaji la ISIS.
Kwa
mujibu wa polisi, kukamatwa kwa wawili hao ambao ni Mwangolo Mgutu na
Abubakar Jillo Mohammed kumezuia mashambulizi ya kigaidi yaliyokuwa
yakipangwa kwa kutumia vilipuzi na silaha nyingine katika mji wa Nairobi
na Mombasa.
Mbali na
kukamatwa kwa washukiwa hao wawili, polisi pia imepata vitu mbalimbali
katika nyumba ya Kiguzo Mwangolo kama vile misumari, betri, waya na
mbolea ambazo inadaiwa zingetumika kutungezea bomu la nyumbani.
Polisi
imeendelea kusema, katika uchunguzi wake wa mwanzo, imebaini kuwa Kiguzo
na Abubakar ni miongoni mwa waandishi wa makala iliyokuwa inasambaa
kupitia mtandao ambao ilikuwa ikielezea kuwepo kwa kundi la Jahba katika
eneo la Afrika Mashariki ambalo limetangaza kumuunga mkono kiongozi wa
ISIS Abubakr Al-Baghdadi.
|
0 maoni:
Chapisha Maoni