Makamu
wa Rais wa Jamhuri uya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan,
akikabidhi Hundi kwa Mkuu wa Mkoa wa Songwe Mhe. Chiku Galawa kwa ajili
ya kukabiliana na uhaba wa Madawati. Jumla ya Madawati Elfu 16.5 yenye
thamani ya Tshs. 1 Bilioni moja zilikabidhiwa kwa Wakuu wa Mikoa
inayozunguka Mbuga ya Hifadhi ya Taifa kwa ajili yakukabiliana na tatizo
la Madawati kwenye Shule zote zilizomo katika Wilaya za Mkoa hiyo.
Makabidhiano hayo yamefanyika leo Mei 16,2016 katika ukumbi wa Ngurudoto
mjini Arusha.katikati waziri wa Maliasili Utalii Profesa Jumanne
Magembe.
…………………………………………………………………………………………..
Mahmoud Ahmad Arusha
Wakuu wa mikoa hapa
nchini wametakiwa kuanza kutenga maeneo ya malisho ya mifugo kwenye
mikoa yao kuepuka mifugo kuingia kwenye hifadhi za taifa na
atakayeshindwa kwenda na maji.
Kauli hiyo imetolewa na
makamu wa raisi Samia Suluhu Hassan wakati akikabidhi madawati kwa wakuu
wa mikoa 19 na wilaya 55 za hapa nchini yaliotolewa na mamlaka ya
hifadhi za taifa Tanapa jijini Arusha.
Alisema kuwa umefika
wakati kwa mikoa iliyokaribu na hifadhi za taifa kuanza kuwadhibiti
wafugaji wanaoingiza mifugo katika hifadhi kwa kisingizio cha kutokuwa
na maeneo ya malisho kuanza mkakati wa kutenga maeneo ilikuokoa
mazingira na uoto wa asili.
Amewataka wakuu hao wa
mikoa kuwa na ukaribu na wahifadhi katika maeneo yao jambo litakalosaidi
kuhifadhi ikolojia ya maeneo ambayo yamekuwa chachu ya kuchangia pato
la taifa.
“Kwa Mkuu yeyote
atakayeshindwa katika hili ajiandae kutumbuliwa jipu kwani hakutakuwa na
msamaha katika hili”alisisitiza makamu wa raisi.
Amesema kuwa msaada huo
uliotolewa uwe chachu ya mabadiliko katika kuhakikisha wanafunzi
wanapata Elimu stahiki bila usimbufu wa kukaa chini na kuweza kuleta
tija katika masomo.
Awali akimkaribisha
makamu wa raising kuongea waziri wa maliasili na utalii Jumanne maghembe
alisema kuwa imekuwa kawaida ya ujirani mwema kati ya hifadhi za taiga
na vijiji kurudisha faida katika miradi inayoibuliwa na wananchi ikiwemo
changamoto ya ukosefu wa madawati na madarasa katika vijiji
vinavyopakana hifadhi zetu za taifa note nchini.
Alisema kutokana na
changamoto hiyo ya kufanikisha upatikanaji wa Elimu bure kwa wanafunzi
kuingia shuleni kwa wingi na kuwa na changamoto ya ukosefu wa madawati
nipo wizara kupitia tanapa wakaja na mkakati huo wa madawati.
Nae mkurugenzi Mkuu wa
mamlaka hiyo Allan Kijazi alisema kuwa shirika hill litatoa madawati 500
kwa wilaya 55 katika mikoa 19 ya hapa nchini ambapo mingi inapitiwa na
hifadhi zetu za taifa.
Amesema lengo kuu in
katika dhana nzima ya ujirani mwema ilikuondoa changamoto mbalimbali
kati ya hifadhi na jirani zao katika kuhakikisha mipaka na uikolokia
unaendelea kuwepo.
0 maoni:
Chapisha Maoni