“Wahenga wanasema penye nia pana
njia na haja ya mja hunena, muungwana ni vitendo.” Hatimae Serikali
imetimiza ndoto zake za kuwa na kituo bora chenye kutoa taarifa za
uhakika zinazohusu masuala ya hali ya hewa katika kiwango cha Kimataifa.
Serikali imeweza kufanikisha
hili kwa kupitia taasisi yake ya Mamlaka ya Hali ya Hewa (TMA) ambapo
mpaka sasa imefanikiwa kuboresha huduma hizo kwa asilimia 80. Haya ni
mafanikio makubwa kutokana na ukweli kwamba kufahamu habari za hali ya
hewa kunasaidia sana kupanga shughuli za kiuchumi na maendeleo.
Hilo limejidhihirisha hivi
karibuni katika taarifa ya tahadhari kuwepo kwa mvua zitakazo ambatana
na upepo kutokana na kuimarika kwa ukanda wa mvua sambamba na uwepo wa
kimbunga Fantala katika Bahari ya Hindi.
Taarifa hiyo ilitolewa na
Mkurugenzi Mkuu Mamlaka ya Hali ya Hewa, Dkt. Agness Kijazi na kusema
mvua hizo zinatarajiwa kunyesha kuanzia Aprili 13-16,2016 ambapo
kutakuwa na mvua kubwa inayozidi milimita 50 ndani ya saa 24. na hili
limetokea kama lilivyotabiriwa. Wenye kuchukua tahadhari wamesha hivyo
na kuepuka madhara yatokanayo na mafuriko. Waliohama baadhi ya sehemu za
mabondeni, walishukuru baada ya kuona makazi yao ya awali yakifunikwa
kabisa na maji.
Mvua hizo zilikuwa zikiathiri mkoa wa Tanga, Dar es Salaam, Pwani,Morogoro pamoja na visiwa vya unguja na Pemba.
Kuthibitisha kuwa kituo hicho
kinatoa taarifa za uhakika ni pale ambapo mwaka jana Dkt. Agness Kijazi
alitangaza kuwepo na mvua za EL-NINO kuanzia mwanzoni mwa mwezi
Septemba–Desemba 2015. Hii ilithibitika baada kushuhudia kuwepo kwa mvua
hizo katika maeneo mbali mbali ya nchi ambapo mvua hizo
zilisababisha mafuriko na uharibifu wa miundombinu,makazi na mazao ya
wakulima.
Utabiri huo wa kuaminika unatokana na TMA kuboresha mtandao wa vituo na usimikaji wa mitambo ya hali ya hewa pamoja na kuongeza idadi ya vituo vya hali ya hewa ambapo vituo vitatu vyenye mitambo ya kisasa vimejengwa katika maeneo mbalimbali ikiwemo Kilwa Masoko- Lindi, Mpanda-Katavi na Songwe.Vituo hivi vimechangia kuongeza upatikanaji wa takwimu na taarifa za hali ya hewa kwa shughuli mbalimbali za kijamii na kiuchumi nchini.
Utabiri huo wa kuaminika unatokana na TMA kuboresha mtandao wa vituo na usimikaji wa mitambo ya hali ya hewa pamoja na kuongeza idadi ya vituo vya hali ya hewa ambapo vituo vitatu vyenye mitambo ya kisasa vimejengwa katika maeneo mbalimbali ikiwemo Kilwa Masoko- Lindi, Mpanda-Katavi na Songwe.Vituo hivi vimechangia kuongeza upatikanaji wa takwimu na taarifa za hali ya hewa kwa shughuli mbalimbali za kijamii na kiuchumi nchini.
Kwa sasaSerikali kupitia TMA
imeanzisha kituo cha kupimia hali ya hewa na Kilimo kiitwacho Agromet
Station hukoMatangutuani Pemba na hivyo kuongeza idadi ya vituo vya
kutoa huduma za hali ya hewa katika sekta ya Kilimo na kufikia vituo 15
nchini,hivyo kuongeza ubora wa taarifa zinazotolewa.
Kwa upande wa taarifa za anga ya
juu Mamlaka imeimarisha huduma za Usafiri wa Anga kwa kuboresha mtambo
wa kupima hali ya hewa katika anga za juu (Modernization of Upper Air
System) katika kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere Dar es
Salaam (JNIA) pamoja na kufufua kituo cha kupima taarifa za anga ya juu
kilichopoTabora.
0 maoni:
Chapisha Maoni