Maafisa
nchini Burundi wanasema kwamba Rwanda imewafukuza zaidi ya raia elfu
moja mia tatu wa Burundi kutoka nchini humo katika kipindi cha wiki moja
iliyopita, baada ya wao kukataa kuhamishiwa hadi katika kambi ya
wakimbizi.
Afisa mmoja amesema kuwa wale ambao walikataa kwenda katika kambi ya wakimbizi, walinyanganywa mali yao na kisha wakafukuzwa.
Makumi
kwa maelfu ya Warundi walikimbilia Rwanda tangu ghasia zilipoanza nchini
mwao mwaka mmoja uliopita, kufuatia uamuzi wa Rais Pierre Nkurunziza wa
kuwania Urais kwa muhula wa tatu kinyume na katiba.
Rwanda pia imewatimua Warundi ambao wameishi na kufanya kazi nchini humo kwa miaka mingi.
|
0 maoni:
Chapisha Maoni