WANAFUNZI wa shule ya Msingi
Ishololo Kata ya Usule Jimbo la Sorwa Halmashauri ya Shinyanga Vijijini
wako hatarini kupata maradhi ya kuambukiza , kutokana na Shule hiyo
kukosa choo kwa kipindi cha miaka mitatu sasa .
Shule hiyo yenye wanafunzi
zaidi ya mia nne (400) wa darasa la kwanza hadi la saba ambao wanatumia
vichaka vilivyoizunguka Shule hiyo kama choo , jambo ambalo linaweza
kusababisha madhara ya kupata magonjwa ya mripuko ikiwemo kipindi
kipindu.
Wakizungumza na mwanadishi wa
habari hizi , baadhi ya wazazi wa wanafunzi wanaosoma katika shule hiyo ,
walisema bado uongozi wa kijiji pamoja na kamati ya shule hawajalipa
kipaombele suala la ujenzi wa Choo katika Shule hiyo.
Aidha waliutaka uongozi wa
Serikali ya kijiji kuweka wazi matumizi ya michango ya wazazi ambao
walichangia kila familia Tshs 2,500/=ambazo hadi sasa hawafahamu jinsi
zilivyotumika kwani tatizo liko pale pale .
Mmoja wa wanakijiji
aliyejitambulisha kwa jina la Kurwa Shija aliliambia gazeti hili kuwa
uongozi wa kijiji pamoja na kamati ya shule wameshindwa kufafanua sababu
zilizokwamisha ujenzi wa choo licha ya kwamba wazazi walichangia
mamilioni ya fedha kwa ajili ya kuliondoa tatizo hilo.
“Kijiji kina familia zaidi ya
mia nne , na kila familia ilichangia Tshs 2,500/= miaka mitatu iliyopita
, lakini hatujui ni sababu gani zimekwamisha ujenzi wa choo , tuna
wasiwasi watoto wetu kupata maradhi ya mripuko ”alifahamisha.
Naye John Salamba akizungumza
kwa masikitiko alifahamisha tatizo hilo lilisababisha baadhi ya wazazi
kufikishwa mahakamani baada ya kukaidi agizo la kuchangia 2,500/= kama
walivyokubaliana .
Aidha aliutaka uongozi wa
Kijiji kuitisha mkutano wa wanakijiji wote ili kujadili hatma ya ujenzi
wa Choo , ambao umekwamba bila ya kutolewa taarifa sahihi na sababu
zilizokwamisha kuanza kwa ujenzi huo.
“Uongozi wa Kijiji uliwahi
kuwafikisha mahakamani baadhi ya wanakijiji wakati wa uchangiaji ,
lakini kwa sasa hatuoni kinachoendelea , hivyo iko haja kwa serikali ya
kijiji kuitisha mkutano ili watueleze wapi walipokwama ”alisema.
Wakizungumzia kadhia ya ukosefu
wa choo , baadhi ya wanafunzi walielezea hofu juu ya usalama wao na
maisha yao , na kuutaka uongozi wa Kijiji na Kamati ya Shule
kuharakisha ujenzi wa Choo ili waondokane na adha ya kutumia vichaka
kujisaidia.
Mwenyekiti wa Serikali ya
Kijiji Juma Panya pamoja na Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo hawakupatikana
kulizungumzia hilo baada ya kudai kwamba wako nje ya Kijiji kikazi na
kutaka watafutwe siku nyin
0 maoni:
Chapisha Maoni