MAELEZO Dar es Salaam
HALMASHAURI za Miji na Wilaya
nchini Miji zimekumbushwa kukamilisha zoezi la upatikanaji wa madawati
kwa shule za msingi na sekondari ifikapo juni 30 mwaka huu ili
kutekeleza agizo lililotolewa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli.
Rai hiyo imetolewa leo na Mkuu
wa kitengo cha Mawasiliano Serikalini katika Ofisi ya Rais Tawala za
Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Rebecca Kwandu wakati wa mahojiano
na mwandishi wa habari hizi kuhusu uchakavu wa madarasa na ukosefu wa
madawati unaozikabili shule za kinesi A na B zilizopo wilaya ya Rorya
mkoani Mara.
“Suala la upungufu wa madawati na
uchakavu wa madarasa ni changamoto ya kitaifa na kwamba lilishatolewa
agizo na mheshimiwa Rais John Pombe Magufuli kuhusu halmashauri zote
nchini kuhakikisha ifikapo Juni 30 mwaka huu kila mwanafunzi anaketi
kwenye Dawati” Alisema Kwandu.
Kwa mujibu wa Gwandu alisema
Serikali ya awamu imepania kuinua kiwango na ubora wa elimu nchini
kupitia mikakati na sera ya elimu bure nchini kote.
Aliongeza kuwa hatua hiyo imeibua
changamoto kubwa kwa wanafunzi wengi kujitokeza kwa asilimia kubwa na
hivyo ni wajibu wa halmshauri hizo kukidhi mahitaji ya madawati ili
wasome katika mazingira mazuri.
“Mpaka sasa Serikali imeendelea
kutoka pesa kwa ajili ya elimu bure nchini kote na kumekuwepo kwa
changamoto mbalimbali kama upungufu wa walimu,madawati na madarasa
ambapo serikali inafanya jitihada za kila namna ili kutatua changamoto
hiyo”
Akifafanua zaidi Gwandu alisema
Serikali inaandaa harambee mbalimbali na kuongeza wigo wa utoaji wa
vibali vya kuchangia maendeleo ya elimu kwa hiari ili kutoa nafasi kwa
wadau mbalimbali wenye nia ya kufanya.
0 maoni:
Chapisha Maoni